Wednesday, May 29, 2013

WIKI YA MAZIWA SONGEA UHAMASISHAJI WA KUFUGA NA KUNYWA MAZIWA UNAENDELEA


Afisa Masoko mwakilishi wa kanda ya nyanda za Juu Kusini wa ASAS, Bw. Jimmy Kiwelu, akiwaelezea watazamaji akiwepo Shani Nachele, (katikati) waliotembelea banda la ASAS bidhaa za maziwa wanazotengeneza ikiwa ni pamoja na Samli, cheese, yoghurt, Maziwa makubwa na madogo na umuhim wa kunywa maziwa yaliyotengenezwa kwakuwa yamepimwa viwango kwa matumizi ya binadamu. Bw. Kiwelu ametahadharisha kunywa maziwa yanayotokana nang'ombe wanaopata tiba huathiri afya ya mtumiaji maziwa hayo kutokana na sumu za dawa.


Maelezo yanaendelea, kibarua cha Bw. Jimy Kiwelu hapo kinaonekana jinsi anavyowakamata watu katika maonyesho ya wiki ya maziwa 29-5-2013 hadi  kilele 1-6-2013 Songea Ruvuma


Maafisa toka Serikali ya Mkoa wa Ruvuma, Mganga wa Mifugo mkoa wa Ruvuma, Dkt. Ramadhani Mwaiganju akifurahia jambo aliloelezwa na Afisa Biashara wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Nehemia james katika viwanja vya manispaa wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 17 ya Wiki ya Maziwa nchini mkoani Ruvuma.


Banda la  Ng'ombe katika viwanja vya maonyesho ya wiki ya maziwa nchini, Songea Ruvuma



Mkurugenzi wa Demashonews.blogspot.com, Bw. Hamza Juma, akiwasiliana na wadau mbalimbali katika banda mojawapo  Viwanja vya Manispaa ya Songea, siku ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya 17 Wiki ya Maziwa nchini, Songea Ruvuma




Kunywa maziwa kwa kwenda mbele, Mzee Nyoni (Small) wa Makambi mjini Songea akihamasika  kunywa maziwa kwa mrija huku Bw. Jimmy Kiwelu akiendelea kuhudumia waliohamasika kunywa maziwa katika banda la ASAS leo mjini Songea 


Mhe. Meya wa manispaa ya Songea,  Charles Muhagama (katikati) akiwa ameongozana na mhe. Diwani toka Morogoro (kushoto) na Afisa mmojawapo wa Halmashauri ya Manispaa Songea kwenda kujionea mazao ya maziwa katika siku ya ufunguzi wa maadhimisho ya 17 ya Wiki ya Maziwa nchini, Songea mkoani Ruvuma leo.


Banda la ASAS linalouza maziwa na bidhaa zake


No comments:

Post a Comment