Wednesday, May 8, 2013

MAADILI YA UMMA YAMETIWA UNAJISI MBELE YA MADHABAHU YA FAIDA


Dkt. Edward Hosea
Na Juma Nyumayo, Songea

TAASISI ya Kuzuia na Kupamabana

na Rushwa nchini, (TAKUKURU ) imesema, maadili ya umma yametiwa unajisi mbele ya madhabahu ya faida.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt. Edward  Hosea,  wakati akitoa mada kwa wanafunzi wanachama wa klabu za wapinga rushwa zaidi ya 70 kutoka sekondari mbalimbali mkoani Ruvuma katika Ukumbi wa Herritage cottage, Mjini Songea.

Dkt. Hosea amesema maadili ya binadamu ni matakatifu kutokana na uadilifu anaotakiwa awe nao, na kudai kitendo cha yeye kutaka faida zaidi hapo ameunajisi kwakuwa faida hizo zimejikita katika fedha chafu, udanganyifu, wizi na bahati mbaya hata huduma zitolewazo kwa jamii hupatikana kwa malipo. 

"Tatizo hili ni mtambuka linalohusisha mambo kadhaa..bali pia linahusu utoaji wa huduma za jamii ambapo huduma hizo zinapatikana kwa malipo," alisema.

Mafunzo haya hapa Songea, ambayo yalianza na Viongozi wa dini wa  mikoa mitatu ya Njombe, Iringa na Ruvuma yameendelea na Klabu za wapingwa rushwa za wanafunzi kwa lengo la kuiwezesha jamii kutambua nafasi na wajibu wao katika mapambano dhidi ya rushwa.

Aidha, mafunzo hayo yatawezesha jamii kutoa taarifa za vitendo vya rushwa TAKUKURU, na kuitokomeza kuanzia ngazi ya mtu binafsi, familia kijiji na hatimaye taifa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment