Tuesday, September 10, 2013

WAANDISHI NA VINGOZI WA SERIKALI

Baadhi ya Waandishi wa habari wanaume wa mkoa wa Ruvuma, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya Mkoa wa Ruvuma. (Mwenye shati la maua katikati) ni  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabith Mwambungu ( jirani yake kushoto )  ni Mkuu wa Wilaya ya Songea,  Bw. Joseph Joseph Mkirikiti . ( Picha kwa hisani ya Ruvuma Press Club)

MTIHANI WA DARASA LA VII - 2013

Tunawatakia wanafunzi wote wa Darasa la Saba (VII) nchini mtihani mwema wa kumaliza elimu ya Msingi. utakaoanza kesho Jumatano 11, September 2013.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa
Mtihani huu utakaofanyika kesho ndio msingi imara utakao amua kuendelea na masomo ya sekondari kwa mwanafunzi muhusika au la.
Miaka hii ya karibuni, tumeshuhudia waziwazi vyombo vyetu vya usalama vimewakamata baadhi ya wanafunzi, walimu na mara nyingine hata wazazi kushiriki kikamilifu katika uhalifu wa kielimu wa kuiba mitihani .
Uhalifu huu unafanywa ili kuwafaulisha wanafunzi wasiostahili na ndio wanaokuwa mizigo katika elimu yao ya upili. Jambo hilo ni baya kupita maelezo kwani elimu ni sawa na moto. Moto haukopeshi, ukiweka mkono katika kaa la moto utaungua mara moja. Na elimu hali kadhalika kama kijana hana uwezo akapitishwa kwa hila kuendelea na masomo, huwa ni mzigo kwa kijana huyo, familia yake pia taifa.
Tusishangae kuona madaktari feki, wahandisi kanjanja, walimu mizigo wanasiasa bomu na wengine kibao bila kusahau wakulima wasiozingatia kanuni za kilimo bora.
Lengo kuu hapa ni kuwatakia mtihani mwema, usio na hila za kuvujishwa wala kuvujisha.
Jamii ya wanaRuvuma inasema hakuna linaloshindikana, utavuna ulichopanda.
Mtihani Mwema 2013