Saturday, August 31, 2013

KISOMO MWANZA WAPETA

Na Juma Nyumayo, Songea
KITUO Cha Taifa Kisomo Mwanza kinaendelea kutoa huduma zake kwa kuzingatia Matokeo Makubwa sasa (Big result Now) Kituo hiki kinaongozwa na Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza, Bibi Mary Salu ambaye amewakaribisha wakuu wa vituo vya uchapaji kanda vya Songea, Mbeya, Tabora na Mkuu wa Press 'A' Dar es Salaam. angalia Picha zifuatazo.
Watumishi wa Kituo cha Kisomo Mwanza wakiwa katika Idara ya Computer, anayeonekana mbele ni Rabeca Fred akiwa kazini.



Mr Andrew Kingu akionyesha Ubora wa kazi zinazochapwa na Kiwanda cha Kisomo Mwanza

Naibu Mkurugenzi Kituo cha  Taifa Kisomo Mwanza, Bibi mary salu ( kushoto) akitoa maelezo kuhusu kiwanda cha uchapaji kisomo mwanza (kulia) ni juma Nyumayo toka Tujifunze Songea.



Friday, August 16, 2013

WAANDISHI WA HABARI RUVUMA WAONYWA

Na Steven Augustino, Songea
WAANDISHI wa Habari Mkoani Ruvuma wameonywa kuamini habari kutoka
mitandao na kuzitumia kuhabarisha umma bila  kuzifanyia utafiti wa
kutosha katika internet na kutumia vyanzo vya kuaminika ikiwemo
kuwahoji wahusika kupata habari za ukweli ambazo zitakuwa na manufaa
kwa wasomaji.
Hayo yameelezwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya
kuandika Habari kwa kutumia mitandao ya Internet na kutuma picha za
kihabari  Mtandaoni yanayoendeshwa katika Ukumbi wa Veta,Manispaa ya
Songea, Taasisi ya Vyombo vya habari kusini mwa Africa (Media
Institute of Southern Africa) MISA TANZANIA.
Wanahabari hao pia wanafundishwa namna ya kufanya utafiti wa vyanzo
vya habari mbalimbali katika Internet na kufungua njia nyingine za
mawasiliano kama  ‘youtube’, Blogu na namna ya kuzitumia katika tasnia
ya kutengeneza na kutuma habari zikiwa na takwimu sahihi.
Awali akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu, Afisa
Habari MISA -TANZANIA , Sengiyuva Gasiligwa,  alisema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kwenda na
wakati hasa katika teknolojia ya kimtandao.
Wanahabari hao pia wananolewa ili waweze kujua kwa undani maana ya
internet, ‘Worid Wide Web’ , ‘Computer’,  na matumizi yake kwa manufaa
ya maendeleo ya technolojia, uchumi, siaa na utamaduni na kujali
maadili
Gasiligwa alisema kuwa mafunzo hayo yanayo wahusisha Waandishi wa
Habari za Magazeti, Terevissin na Radio yanafanyika kwa ushirikiano
MISATAN na shirika la VIKES  toka Finland na kwamba kwa kuanzia
mafunzo hayo yalifanyika Mkoani Pemba huku Zanzibar Tanzania Visiwani
na sasa Ruvuma na baadaye mkoani mwanza.
Nae mwezeshaji wa mafunzo hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini
Iringa,  Saimon Berege,  pamoja na mambo mengine aliwataka Wanahabari
hao kuwa na ari ya kujiendeleza kielimu na kuwakaribisha kwenda kusoma
digrii ya pili (masters) Inayotolewa na chuo hicho.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wanahabari hao pamoja na kuipongeza
taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari
wamesema kuanzia sasa wataweza kufanya kazi za uandishi wa habari wa
kiuchambuzi kwa kuoanisha habari kutoka vyanzo vya mataifa mbalimbali,
kuandika habari kwa kutumia takwimu kutoka katika mitandao na kutumia
taarifa na hotuba zilizopita zilizotolewa na viongozi wa mataifa
mbalimbali duniani .
Aidha washiriki hao wameonyesha ushirikiano mkubwa katika uchambuzi wa
mada zilizotolewa na wameomba mafunzo kama hayo yatolewe mara nyingi
iwezekanavyo ili kuwakumbusha kuamsha ari ya waandishi.
Mwisho