Friday, May 3, 2013

BREAKING NEEEEWS!!!! YA MWAKA, SERIKALI IMEFUTA MATOKEO YA KIDATO CHA IV 2012,





Waziri Wiliam Lukuvi.


Na Juma Nyumayo, Dar es Salaam,

SERIKALI imefikia uamuzi wa kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2012, na kutoa maelekezo kwa Baraza la Mitihani kurekebisha alama za wanafunzi hao kwa kufuata utaratibu uliotumika mwaka 2011.

Hayo yamejiri leo Bungeni, na kupokelewa kwa mshangao na wadau mbalimbali hapa nchini wakiongozwa na wanafunzi wenyewe, wazazi na walimu. Watu wengi waliumizwa na matokeo hayo yaliyopelekea serikali kuunda Tume ya kuchunguza mdororo huo na changamoto nyingine kibao.
Hatuna uhakika kama hayo ni baadhi ya matunda ya Tume hiyo ya kufutwa kwa matokeo ya Mtihani huo yaliyoiletea aibu na fedheha Tanzania.

Aibu hii ni ile iliyowafanya watu mbalimbali kuchukua uamuzi wa kusema kuna muanguko na mdororo wa elimu Tanzania. Wakiongozwa na Mhe. Mbatia wa NCCR, na viongozi wa upinzani Bungeni lakini hata katika ngazi ya familia watu wanashindwa kuangaliana usoni kwa matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Matokeo hayo hayakujali unasoma shule ya kiwango gani, ikaacha waliopata 'zero' kama Laki mbili hivi na wachache sana kupata division I.

Kwa mujimu wa maelezo ya Waziri Wiliam Lukuvi, 'standardization' ya  alama zitafanyika na huenda vijana hao ambao wengine wametangulia mbele ya haki, kuathirika kisaikolojia na mengine mengi wakafarijika na kujikuta katika nafasi nzuri.
Tutaendelea kuwaletea habari zaidi.




No comments:

Post a Comment