Kamanda Nsimeki akionyesha Pembe za Tembo leo |
JESHI la Polisi kwa mara nyingine tena Mwezi huu limekamata Pembe za Tembo zenye thamani ya shilingi milioni 8,398,000 kutoka mtandao wa majangili wa Kijiji cha Mandepwende wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, amemuambia mwandishi wa habari hizi nje ya Ofisi yake kuwa yeye na Kikosi cha kuzuia Ujangili Kanda ya kusini wamejipanga vizuri na ndio maana Mtandao wa Majangili umebanwa kila kona.
"Nakuambia hawa tutawabana kila kona, maana nakili kuwa tunafanya kazi kwa uelewano mkubwa na kikosi cha Kuzuia ujangili kanda ya kusini," alisema Kamanda Nsimeki akitamba kuwa sasa ndio Arobaini yao.
Alisema ametoa wito kwa wanchi wema kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama na pia kuwatahadharisha wote wanaojihusisha na biashara hiyo waache mara moja.
Pembe za ndovu zilizokamatwa ni 11 ambazo ni sawa na Tembo sita ambao wameuawa na majangili hao.
Hivi karibuni, jumuia za kimataifa zimelaani biashara ya pembe za tembo ambazo zimesababisha kuuawa kwa Tembo wengi hapa Afrika. Miongoni mwa mataifa yanayolaumiwa zaidi ni pamoja na nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikiwa mojawapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki akiwaonyesha waandsi wa Habari (Hawapo pichani) Pembe mbili za ndovu miongoni mwa zilizokamatwa zenye Thamani ya Shilingi milioni 8,893,000. Pembe hizo zote zimekamatwa Kijiji cha Mandepwende wilayani Namtumbo.
No comments:
Post a Comment