Sunday, May 12, 2013

ANGALIA UZURI WA ANGA, UPINDE WA MVUA (RAINBOW)

Upinde wa mvua ukionekana una hadithi na simulizi mbalimbali katika jamii za kiafrika. Wengine husema Simba jike anazaa, na maelezo kadhaa wa kadhaa. Watoto hasa wanafunzi hupenda sana kufikia eneo lenye rangi hizo ili kushuhudia kama zinashikika au la, kwa utukutu wao. Naamini hata wewe msomaji uliwahi kufanya utafiti huo na kuuliza ni nini hasa kinafanya rangi hizo zijitokeze angani?  majibu mengi ulishapewa.
Ukweli ni kwamba Jambo hilo ni la kisayansi zaidi kwamba matone ya mvua (maji) yakipenyesha mwanga na kupindishwa (refraction of light) hutokea hizo rangi saba. 
Upinde wa Mvua, umeonekana jana maeneo ya milima ya Matogoro, Manispaa ya Songea jana na kulipamba anga kwa rangi kwa kiingereza naziweka hapa (ROYGBIV) - Red, Orange, Yellow, Green, Blue, Indigo and Violet. angalia mpangilio huo katika picha nyingine hapo chini. (Picha, Maelezo na Juma Nyumayo)





Hiyo ni picha iliyovutwa kwa karibu ya upinde wa Mvua iliyopigwa jana hapa manispaa ya Songea nyuma ya Mtaa wa Karibu na Bar ya Serengeti , jana.


No comments:

Post a Comment