Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel
Nchimbi akizungumza na mmojawapo wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya
waliofanya kikao naye jijini Dar es Salaam Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
IJP Said Mwema.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Kikao na Wawakilishi wa Nchi
za Umoja wa Ulaya waliomtembelea Wizarani.. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema, pia
alihudhuria Kikao hicho akiwa na Wakuu wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam
(Kushoto).Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
---
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel
nchimbi amesema Serikali imeimarisha shughuli za ulinzi hapa nchini ili
kuhakikisha kuwa wananchi na wageni wanaishi na kufanya shughuli zao kwa
amani.
Dk. Nchimbi ameyasema hayo leo jijini Dar es
Salaam alipokutana na Ujumbe wa wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na
baadhi ya mabalozi wa Nchi hizo waliopo hapa nchini.
Aliuambia ujumbe huo ulioongozwa na Balozi
Filberto Cerani Sebregondi kuwa Jeshi la Polisi limeweka mikakati mbalimbali ya
kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na maeneo
mengine ya nchi.
Amesema kwa upande wa raia wa kigeni, Jeshi hilo
limeanzisha Dawati Maalumu litakalohudumia raia hao pale wanapopata matatizo ili
waweze kupata huduma za haraka.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo amesema
Umoja huo utaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na
ameishukuru Wizara hiyo kwa jitihada inazoendelea kuchukua kuhakikisha ulinzi na
usalama unaimarishwa kwa wageni na raia
No comments:
Post a Comment