Thursday, May 2, 2013

VIONGOZI WA ASASI WAKUTANA DAR KUJADILI UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA


Mwezeshaji wa mada ya Uanzishwaji wa Mabaraza ya Katiba " Vipi NGOs zinaweza kuanzisha na kuendeleza mabaraza ya Katiba? " Gloria Mafole,  toka Kituo cha  Sheria-  LHRC, Dar es Salaam, (Kushoto)  akishauriana na Afisa toka The Foundation for Civila Society, Neema Yobu Ukumbi wa Blue Pearl ambako wajumbe toka Mitandao ya wilaya ya  Asasi za kiraia wakiendelea na Mkutano. (picha na Juma Nyumayo) 


Bw. Juma Nyumayo, (katikati) akishauriana jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba, (Kulia0 ambaye alitoa mada ya Uzoefu wa Jukwaa la Katiba katika kuweka mazingira mazuri ya uhusishwaji wa wananchi / makundi maalum katika Mabaraza ya Katiba  wakati Bw Mathew Ngalimanayo (Kushoto) akifuatilia na kufurahishwa na hoja leo katika Ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza Dar es Salaam.. (Picha na Juma Nyumayo)


Kama hapo juu, na hiyo picha ya chini zinavyoonyesha mjadala ukiendelea wa wanaharakati hao leo.


No comments:

Post a Comment