Moja ya nyumba zulizochomwa moto |
Nathan Mtega,Songea
BAADHI ya waandishi wa habari na wadau wa habari
mkoani Ruvuma wamelaani vitendo vya ukatili dhidi ya waandishi wa habari
vilivyofanywa na baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mtwara ikiiwa ni kuwazuia kufanya
kazi yao kwa uhuru ya kuhabarisha ikiwa pamoja
na kuchoma moto nyumba na gari la mwandishi wa habari wa kituo cvha utangazaji
cha taifa.
Wakizungumza na Radio One Stereo kwa nyakati
tofauti baadhi ya wakazi hao wa mjini Songea walisema kuwa vitendo vya namna
hiyo mbali ya kuhatarisha usalama wa waandishi wa habari lakini pia vimekuwa
vikiwaathiri kisaikolojia na kiuchumi kwa sababu wanajengeka na hofu ya usalama
wao.
Akizungumza mmoja wa wadau wa habari Anthon
Ngonyani mkazi wa mjini Songea alisema kuwa waandishi wa habari ni miongoni mwa
watu muhimu katika jamii kwa sababu mchango wao ni chachu ya maendeleo ya jamii
nzima na kwa maslahi ya taifa zaidi
hivyo kila mmoja ana wajibu wa kujali mchango wao na siyo kuwadhoofisha kwa
namna yoyote.
Naye Mwandishi wa
habari Juma Nyumayo alisema kuwa habari ni hewa ya oksijeni ya maendeleo ya
nchi na ili waweze kuelekea kufanya shughuli zao kwa usahihi ikiwa watapata
ushirikiano wa waandishi wa habari na jamii husika na kitendo cha baadhi ya wananchi hao kuwazuia
au kuwadhuru waandishi kufanya kazi yao ni sawa na kumziba mtu kupata hewa hiyo
muhimu.
Aidha hivi karibuni
kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa kuwashambulia kwa
maneno waandishi wa habari wa baadhi ya vyombo vya habari jambo ambalo
linapandikiza chuki baina ya wananchi na waandishi wa habari na kusababisha
baadhi yao
kushambuliwa au kutishwa.
Akizungumza mmoja wa
viongozi wa dini mjini Songea ambaye hakutaka jina lake litajwe
alisema kuwa ni vyema mamlaka husika zikaona umhimu wa kuzuia vitendo hivyo visiendelee
kujitokeza kwa kuziba mianya ya kutokea badala ya kusubiri vitokee ndipo hatua
zichukuliwe na vikiachwa utageuka utamaduni wa kuwadhuru.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment