Monday, May 13, 2013

RUVUMA INAKABILIWA NA UPUNGUFU MKUBWA WA WAUGUZI

Mhe Said Thabit Mwambungu
Na Juma Nyumayo, Songea
WAUGUZI mkoani Ruvuma wameilalamikia serikali  kwa upungufu mkubwa wa watumishi wa kada yao mkoani Ruvuma, jambo ambalo linawafanya wabebe mzigo mkubwa wa kazi na lawama toka kwa wananchi wanaowahudumia.
Malalamiko hayo yalisomwa  katika Risala ya wauguzi wa Mkoa wa Ruvuma mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu, aliyekuwa mgeni rasmi wa maadhimisho siku ya wauguzi kimkoa katika viwanja vya Manispaa ya Songea  jana.
Mkuu wa Mooa Mwambungu alisema wauguzi sharti wasikilizwe kilio chao na serikali pamoja na wadau wengine wa afya sharti wasaidie kuziba pengo hilo kwakuwa fani hiyo ni muhimu sana.

Siku hiyo ambayo kitaifai iliadhimishwa mkoani Rukwa,  hapa mkoani Ruvuma imeadhimishwa katika Manispaa ya Songea  na wauguzi walivaa sare ya T-Shirts nyeupe  ' Maarufu kama Form Six"  na surualia au "skirt" nyeusi chini, wakianza na maandamano na baadaye kupitia risala na michezo ya kuigiza walisema wanaupungufu wa wauguzi 1,628 sawa na asilimia 68.8.
Kwa lugha nyepesi ni kila wanapohitajika wauguzi 10 ni watatu tu wapo kazini.
Kilio hiki kilikwenda sambamba na mchezo wa Kuigizwa ulionyeshwa hapo katika viwanja vya Manispaa ya Songea ambapo  Muuguzi mmoja akionyeshwa anakabiliwa na wagonjwa zaidi ya nane kila mmoja akimlilia na kumtajia asaidiwe.
Hali hiyo ilimuacha muuguzi akichanganyikiwa na kushindwa kutoa huduma tarajiwa na kuonyesha ni namna gani wauguzi waliopo mkoani Ruvuma wanavyokabiliwa na changamoto hiyo ya upungufu wa wauguzi katika vituo vya kutolea tiba.
Aidha wauguzi hao, walitumia maadhimisho hayo kuwaonya vijana na wazazi kutowapeleka katika vyuo visivyosajiliwa vya kusomea kazi hiyo.
" Mheshimiwa mkuu wa Mkoa, hivi sasa kumezuka vyuo vingi vya kusomea kazi ya uuguzi feki, napenda kuwaqjulisha kuna jumla ya vyuo 73 hapa nchini vinavyotambulika," alisema Muuguzi Mkuu wa Ruvuma na kubainisha kuwa Vyuo hivyo vinatoa mafunzo kuanzia ngazi ya Cheti, Stashahada, Astashada na Shahada.
Hali halisi ya matibabu na huduma za Afya mkoani hapa hasa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma inalalamikiwa na wagonjwa na ndugu wa wagonjwa kwa kukosa dawa markwamara.
Uchunguzi umebaini bajeti ndogo na kuelemewa kwa wagonjwa wanaokwenda Hospitali hiyo kama ya Rufaa na baadhi ya wagonjwa wa Manispaa ya Songea kutohudhurioa katika Kituo cha Afya cha Mjimwema ni mwiba mwingine katika Hospitali hiyo maarufu kama Hospitali ya Mkoa ya Songea (Homso)
Taarifa toka Homso zinasema ili waweze kutoa Tiba kwa wastani mzuri dawa na vifaa tiba vya Shilingi milioni 45 huhitajika kwa mwezi mmoja.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Benedikt Ngaiza, mwanzoni mwa Mwaka huu aliwahi kunukuliwa akisema ufinyu huo wa bajeti huwakumba mara kwa mara na huletewa pesa pungufu kwaajili ya dawa na vifaa tiba.
"Mwezi Oktoba 2012 tulipokea Shilingi milioni 35 tu badala ya Shilingi Milioni 45, " alisema Mganga. Mfawidhi wa Homso, Dkt Ngaiza .

No comments:

Post a Comment