Tuesday, May 14, 2013

BEI YA KUZIONA YANGA V/S SIMBA - JUMAMOSI HII

Nembo za Yanga na Simba

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000.Kiingilio hicho kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa akiba ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Leslie Liunda.
 
KOCHA KIM KUZUNGUMZIA MECHI YA MOROCCO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tiketi kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco. Mkutano huo utafanyika keshokutwa (Mei 16 mwaka huu) saa 5 kamili kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu kwenye jiji la Marrakech nchini Morocco. Taifa Stars ilishinda mechi yake iliyopita jijini Dar es Salaam kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Morocco.
 
Angetile Osiah
Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 
Source:  via lukwangule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment