Mhe. Samuel Sitta
WAZIRI wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta, amesema wakati ukifika, yeye na
rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe,
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Dk. John Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dk Harrison Mwakyembe,
watachagua mmoja wao watakayeona anafaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa
2015.
Waziri Sitta
aliyasema hayo jana katika Kongamamo la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la
wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT),
Mwanza.
Mara ya kwanza,
Sitta aliwataja rafiki zake hao juzi wakati wa harambee ya kuchangia Kanisa
Katoliki, Josephine Bakita, Parokia ya Igoma, Mwanza.
Pia alisema
hatagombea tena Ubunge Urambo ya Mashariki baada ya kuwa katika ulingo wa siasa
kwa miaka 35 na badala yake ataangalia namna nyingine ya kuwatumikia wananchi
huku akigusia mchakato wa kuwania urais ambao, alisema anamwachia
Mungu.
“Kwa ubunge
nimekwisha waeleza inatosha sitagombea tena kwani miaka 35 inatosha, … lakini
hatima yangu ni nini siwezi kujua lakini nina afya nzuri na mmoja wa wanasiasa
wakongwe, wenye afya nzuri, mnaona ninavyopendeza... kwa urais namwachia Mungu
tutaona,” alisema Sitta.
Alisema yeye
rafiki zake hao wana mawazo yanayolingana katika mustakabali wa nchi hii na
kwamba wataendelea kutembea sehemu mbalimbali za nchi kuwajengea wananchi uelewa
ili wajue kuwa uongozi ni lazima ukae katika mikono salama.
“Tutaendelea
kupita katika nchi hii kuwaeleza wananchi kujua uongozi wa nchi hii lazima ukae
katika mikono safi na ikitokea mmoja wetu akatamani urais, basi tutaona
inavyofaa, lakini tutasubiri watu wanavyosema pia kuhusiana na nasi,”
alisema.
Akijibu swali
la mwanafunzi wa SAUT kuhusiana na kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete wakati wa
Uchaguzi Mkuu uliopita ilhali akijua kwamba hawezi kuwaletea maisha bora
wananchi, alisema kwake ilikuwa ni sawa na kuchumbia na kwamba wakati wa
uchumba, mchumba huonekana kuwa bora lakini anaweza kubadilika wakati wa
ndoa.
“Sikufanya kosa
kuwa katika mtandao wa Rais Kikwete, hii ni sawa na kuoa. Unachumbia. Mchumba
hawezi kuwa sawa wakati wa ndoa au wa kuwa mke, inawezekana katika kugombea mtu
akawa sawa lakini baadaye akajifunua zaidi mambo yake, huwezi kumjua zaidi mtu
labda uwe na Umungu,” alisema Sitta na kusema: “Hata wapiga kura huwakuta hilo
kwa kuchagua mtu ambaye huenda kinyume na matarajio yao.”
Hata hivyo,
alisema kauli hiyo haina maana kwamba Rais Kikwete hakufanya kitu, bali amefanya
mambo mengi na kusema uzuri wa uongozi unapimika wakati anapotoka madarakani
hasa pale historia inapoandikwa na kulinganishwa na marais wengine wajao na
waliopita.
Katika
kongamano hilo la SAUT, Waziri Sitta alifuatana na kada wa CCM, Paul
Makonda.via: mtandao-net
No comments:
Post a Comment