Vifaa vya Umeme Jua |
Na Steven Augustino, Tunduru
WAKAZI wa
Kijiji cha Tinginya, tarafa ya Nakapanya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wamelipuka kwa furaha baada ya kupata umeme kwa mara ya kwanza tangu dunia iumbwe kijini kwao.
Kwa namna ya pekee wakazi hao, wameipongeza
Serikali kwa kuwafungia Mfumo wa Umeme Jua (SOLA) katika Zahanati yao na
kueleza kuwa mradi huo utawakomboa wanawake ambao kwa muda mrefu walikuwa
wakijifungua wakiwa gizani.
Kwa nyakati tofauti, wakazi hao wakiongozwa na Fatuma
Mapila na Bw. Aliahad Abdalahman ambao walikuwa wamepeleka mtoto wao kwa ajili
ya matibabu na Muuguzi wa Zahanati hiyo, Grolia Lupindo ni miongoni mwa baadhi ya
wananchi ambao walishindwa kuzuia furaha yao baada ya kushuhudia wakati mfumo
huo ukiwashwa katika zahanati yao na katika nyumba ya Mganga wa zahanati
hiyo.
Wakifafanua taarifa hiyo walisema
kuwa kwa muda mrefu tangu Zahanati yao ifunguliwe mwaka 1990 hadi
siku hiyo wanawake wa Kijiji hicho na vitongoji jirani walikuwa wakitumi vijinga
vya moto kumulikia wakati wa kujifungua ama kujifungua katika giza hali ambayo
ilikuwa ikihatarisha maisha yao na watoto wanao jifungua.
Awali akiongea na
wananchi hao afisa mafunzo na ujengaji wa uwezo kutoka wakala wa nishati
Vijijini (REA) Mary Ngusaru alisema kuwa ufungaji wa mfumo uliofanywa na kundi
la vijana 35 walio maliza mafunzo ya siku 7 na kwamba hivi sasa Wilaya ya
tunduru imepata hazina ya mafundi wengi wenye uwezo wa kufunga na kufanya
matengenezo madogomdogo ya mfumo huo wa meme jua.
Bi.Ngusaru aliendelea kufafanua kuwa hadi
kuamilika kufungwa kwa mfumo huo na mfumo mwingine utakaofungwa katika Zahanati
ya kijiji cha Nampungu utaghalimu jumla ya shilingi Milioni 20
ambazo zimegahilimiwa na serikali kupitia mpango wa changamoto za milenia (MCC)
na kwamba serikali inaamini kuwa miradi hiyo itatunzwa na kusaidia kupunguza
uhalibifu wa misitu kwa ajili ya matumizi ya nishati ya kuni.
Nae
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mhandisi Philbert Beyanga, kutoa kampuni ya Solar
Energy alisema kuwa katika kipindi hicho vijana hao watanolewa na kupatiwa
ujuzi na uendelezaji wa teknolojia za umeme jua,nishati upepo,nishati
tungamotaka na nishati ya moromoko madogo ya maji.
Alisema
mfumo huo unao uwezo wa kuwasha taa 36 pamoja na kumudu kuendesha
mashine za kupimia malaria hali ambayo itawarahisishia kazi watumishi wa
zahanati hiyo.
No comments:
Post a Comment