Wednesday, May 8, 2013

DKT. HOSEA AMALIZA KAZI RUVUMA, AWATAKA WALIMU NA WANAFUNZI KUPINGA RUSHWA KWA KUANZIA SHULENI KWAO


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, (kushoto) akiwa ameshikana Mkono na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mdandamo (katikati) na Mwenyekiti wa Marafiki wa Elimu Songea, Bw. Juma Nyumayo (kulia) kuonyesha ishara ya nguvu za pamoja kupambana na rushwa mara baada ya kumaliza kufundisha wanachama wa Klabu za wapinga rushwa zaidi ya 70 na walimu wao kutoka shule za sekondari Mkoani Ruvuma leo. Mkurugenzi huyo amerejea jijini Dar es Salaam, baada ya kuwa katika kazi ya kutoa mafunzo kwa viongozi wa Dini mikoa ya Njombe Iringa na Ruvuma na wanafunzi wa sekondari.

Wanakwaya wanachama wa Klabu ya Kupinga Rushwa toka Shule ya Sekondari ya  Wasichana Songea wakipata maelezo toka Afisa mchunguzi wa Takukuru mkoani Ruvuma, Bertha Madili, baada ya kuimba vizuri wimbo wa kupambana na Rushwa na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la kupambana na Rushwa barani Afrika, Dkt Edward Hosea, ambapo walizawadiwa Shilingi milioni moja taslimu.





Baadhi ya wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani Ruvuma, wakipeana mkakati wa namna ya kuboresha klabu za wapinga Rushwa katika shule zao mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku moja katika Ukumbi wa Hoteli ya Herritage Cottage . Mkuu wa Shule ya Sekondari Songea, Mwl. John Sweke, (kushoto) akitoa mkakati wake


Mkakati unaendelea kuwekwa nje ya Ukumbi


Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari  wakiongea hili na lile nje ya ukumbi wa mkutano


No comments:

Post a Comment