Na Nathan
Mtega,Songea
JAMII nchini imetakiwa kujenga
utamaduni wa kunywa maziwa badala ya kutumia fedha nyingi kwenye unywaji wa
pombe ambao hauwashirikishi watoto ambao wanakosa lishe bora kwa sababnu baadhi
ya wazazi wamekuwa wakutumia fedha nyungi kwenye ulevi na kuwasahu
watoto wao.
Alisema kuwa hali hiyo inaonyesha kuwa kasi ya
wananchi kunywa maziwa bado ni ndogo hivyo kunahitajika jitihada za makusudi ili
kuwafanya wananchi kuona umuhimu wa kila mmoja kunywa maziwa kwa sababu maziwa
ni lishe na ufugaji bora wa n g’ombe wa maziwa unaboresha kipato kwa kila
mwananchi na taifa kwa ujumla na huboresha afya ya mlaji wa maziwa bora
yaliyosindikwa kwa ustadi mzuri wa kuzingatia kanuni za afya.
Akizungumza kwenye kilele
hicho cha maadhimisho ya kumi na saba ya wiki ya maziwa nchini Waziri wa mambo
ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la Songea mjini Emmanuel Nchimbi elimu
alizitaka mamlaka mbali mbali kuendelea kutoa elimu ya usindikaji wa maziwa ili
yaweze kushindana kwenye soko nla ndani na nje kwa ajili ya manufaa ya
wasindikaji na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa maziwa mbali ya
kuwa ni moja kati ya vyanzo vya mapato kwa wafugaji lakini pia ni chakula muhimu
kwa kila mmoja kwa ajilki ya kuboresha afya hivyo ni vyema kila mmoja akajenga
utamaduni wa kunywa maziwa zaidi kwa sababu mpaka sasa kiwango cha watu kunywa
maziwa ni kidogo ikilinganishwa na idadi ya ng’ombe wa maziwa waliopo nchini
pamoja na kuwa idadi ya ng’ombe wa kienyeji na wa maziwa.
Akizungumzia kuhusu uhaba wa
ng’ombe wa maziwa nchini alisema kuwa serikali inaendelea kukabiliana na
changamoto hiyo kwa kuongeza jitihada kwenye upatikanaji wa vifaa vya
kuwawezesha wataalamu wa mifugo nchini ikiwa ni pamoja na ifugaji bora kwa
ng’ombe bora ambao wakifugwa na kutunzwa ipasavyo huweza kutoa maziwa mengio
yenye ubora zaidi.
Aidha aliwataka wananchi wa
vijiji vyenye ng’ombe wa maziwa wajiunge kwenye vikundi ili iwe rahisi kuwafikia
na kuwasaidia kimafunzo na halmashauri husika zigharamie gharama za nafunzo hayo
ikiwa ni pamoja kuongeza vifaa vya uhamilishaji wa ng’ombe ili waweze kutoa
maziwa mengi.
No comments:
Post a Comment