Wednesday, June 19, 2013

HII NDIYO TANZANIA TUNAYOITAKA? ARUSHA VURUGU TUPU

 
Vurugu, kamatakamata, mabomu na mshikemshike. Angalia Uwanja wa Soweto mkoani Arusha ulivyogeuka na majanga yake. 
   Moto  ukiwaka katikati ya barabara wakati wa vurugu zilizotokea katika viwanja vya SOWETO mjini Arusha.
Baadhi  ya watu wakifunga barabara baada ya kutawanywa na Polisi kwa mabomu  ya machozi katika viwanja vya SOWETO vilivyopo jijini hapa, Barabara Kuu inayopitisha magari ya mikoani eneo la Kimahama
Moto  uliowashwa na baadhi  ya watu wakifunga barabara baada ya kutawanywa na Polisi kwa mabomu  ya machozi katika viwanja vya SOWETO vilivyopo jijini hapa, barabara iliyopo eneo la Kaloleni.
 Sehemu ya Umati na wananchama na mashabiki wa chadema waliojitokeza viwanja vya Soweto mjini Arusha kuaga miili ya watu walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa Chadema
Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida  Masharik (Chadema ) Mhe.Tundu lissu, akihutubia sehemu ya maelfu ya wapenzi wa  Chadema waliojitokeza viwanja vya Soweto mjini Arusha kuaga miili ya watu walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa Chadema
 Wanafunzi wa shule wakijiziba na nguo na kunawa uso baada ya kudhuriwa na mabomu ya machozi yaliyopigwa leo na Polisi waliokuwa wakitawanya  maelfu ya watu waliokuwa kwenye mkutano katika viwanja vya SOWETO.
Askari Polisi wakilinda uwanja wa Soweto mjini Arusha muda mfupi baada ya kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chadema waliojitokeza waliyojitokeza viwanja vya soweto mjini arusha kuaga miili ya watu walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu uliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa chadema. (Picha  zote na Ferdinand Shayo)
---
Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na watu wengine 60 huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili  wa chama hicho na watu wengine.

Kamishina wa Operesheni wa Mafunzo wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amesema licha ya watu hao kukamatwa pia wamekamata pikipiki 106 na baiskeli 16 ambazo zilitelekezwa.

Chagonja amewataja wanne hao waliotiwa nguvuni kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha
Akonay (Mbulu) Said Arfi (Mpanda Mjini) na Joyce Nkya (Viti Maalumu).

Chagonja amesema limewatia nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika viwanja vya Soweto (al maarufu viwanja vya AICC) jijini humo mwishoni mwa wiki.
  • Taarifa iliyonukuliwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, inasema kuwa uchunguzi wa haraka umebaini kuwa bomu lililotumika kulipua katika mkutano huo wa CHADEMA hivi majuzi limetengezwa nchini China, na aina hiyo ya mabomu yanamilikiwa na vyombo vya dola, hasa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Makosa mengine ni wanayotuhumiwa kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.

Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.

Wanaotafutwa ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.

Wabunge wengine wanaotajwa kuwepo uwanjani hapo ni pamoja na John Mnyika na Ezekiah Wenje.
via/demashonews

No comments:

Post a Comment