Monday, June 3, 2013

WABONGO NA WADAU WAFANYA KWELI KUAGA MWILI WA NGWEAR SAUZ

Angalia picha  namna Marehemu Ngwea alivyoagwa nchini Afrika Kusini, June 2013.

.
Baada ya kutoka kwenye Mochwari ya serikali ya Hillbrow  Johannesburg, mwili wa Ngwea ulihifadhiwa hapa ambako pia msafara wa kwenda kumuaga ndio ulianzia hapa.
Ni zaidi ya Watanzania 50 waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Ngwea akiwemo Msanii Bushoke, Mwamvita Makamba, Kinje Ngombale Mwiru pamoja na Watanzania wengine waliokuja kutembea na wanaoishi na kufanya kazi Afrika Kusini.
Marehemu Ngwea alifariki dunia Mei 28, 2013 Johannesburg South Afrika alikokuja kufanya show, ambapo kilikua ni kifo cha ghafla kwa sababu usiku kabla ya kulala aliagana vizuri na Watanzania wenzake kijiweni tena akaahidi kurudi Afrika Kusini baada ya kipindi cha Ramadhani.
Kabla ya kifo chake tayari Ngwea alitakiwa kurudi Tanzania lakini akaahirisha safari yake mara tatu mfululizo ili aendelee kuwepo Afrika Kusini ambako alimwambia Bushoke kwamba amepata mtu wa kumlipia ada hivyo angerudi Afrika Kusini hivi karibuni ili aanze masomo ya muziki.
.
.
.
Gari la Ubalozi wa Tanzania lililotoka Pretoria likiwa na Mwakilishi wa Ubalozi huo, hapa lipo kwenye msafara kuelekea kanisani kuuaga mwili wa Marehemu.
.
.
.
Msafara wa magari ya Watanzania mbalimbali.
.
Baadhi ya Watanzania wakiubeba mwili wa Marehemu kuuingiza ili kwenda kuagwa.
.
.
.
Josh Kalisa, Habibu Awesi ambae ni mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini, Kinje Ngombale Mwiru na Mwamvita Makamba wakiwa nje ya kanisa alikoagwa Marehemu Ngwea Johannesburg June 3 2013.
.
.
.
.
.
Watanzania wakiingia Kanisani kuaga.
.
.
.
.
.
.
.
Magari waliyokuja nayo Watanzania mbalimbali.
.
Baada ya kuaga, mwili ulipakizwa kwenye gari ili kupelekwa Airport.
.
Ndani kanisani.
.
Huyu ni Ramadhani, ndio Mtanzania ambae alikua anamuendesha Ngwea mara nyingi sana kipindi hiki alipokuepo Johannesburg ambapo usiku kifo kilipotokea, walikoswakoswa kwenye ajali kadhaa barabarani…. hapa alikua anasali kwa ajili ya Marehemu.
.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania akiongea baada ya sala ya kumuombea Marehemu Kanisani.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
VIA/millardayo.info

No comments:

Post a Comment