Thursday, June 20, 2013

MABADILIKO YA HALI YA HEWA YATAATHIRI UTALII NYASA?

Washiriki Mdahalo wa wazi wa mabadiliko ya Hali ya hewa na Tabia nchi iliyoendeshwa na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Ruvuma (RUNECISO) kwa Ufadhili wa The Foundation for Civil Society  wakionyesha Jiwe maarufu la Pomonda lililotumika na babu zetu kujificha wakati wa vita kuu ya Dunia na zile za makabila. Jiwe hilo sasa linaonyesha wazi michirizi inayoonyesha kina cha maji cha Ziwa Nyasa kimepungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi kunakosababishwa na uharibifu wa kibinadamu katika vyanzo vya maji misitu ya Milima ya Livingstone (Milima ya Umatengo) kulikolalamikiwa na washiriki wa mdahalo huo uliofanyika 15/6/2013 Liuli.  
 

Askari Polisi wa anayejulikana kwa jina la Rudo huko Liuli akipanda Mlima akipita katikati kuelekea shule ya Sekondari ya St. Paul. Msitu huo unaotunzwa kwa mara nyingine baada ya miti mingi kukatwa hasa miti ya mipera.
Zamani msitu huo ulikuwa na wanayama wengi wakiwemo Nyani, Ngedele,  Mbega weupe na ndege anuwai ambao hivi sasa wamepotea kutokana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa. 
 

Jiwe la Pomonda likionekana toka Mlimani katika shule ya Sekondari ya St. Paul Liuli wilaya ya Nyasa.
 
 

Safari ya kuelekea Jiwe la Pomonda inaendelea, Pichani ndani ya Boti ni Juma Nyumayo na Judith Lugoye kwa nyuma wakiangalia  mistari hiyo katika mawe inaonyesha kina cha maji kilivyokuwa miaka zaidi ya 50-100 iliyopita na kudhihirisha kuwa kina cha maji kimepungua.
 

Boti limefika Jiwe la Pomonda, Rasta Joseph Ndomondo Tour Guide na Mmiliki wa Pomonda Raha Beach & Campsite (aliyevua shti) akivuta Boti lisimame na abairia watalii wa ndani wateremke, huyo anayeteremka ni Francis Mlimira.
 

Wameteremka watu kadhaa, sasa zamu ya Makamu Mwenyekiti wa RUNECISO, Bw. Adam Nindi, ambaye kitaluma ni Mwandishi wa habari anayeripoti Redio Free Afrika na Star TV kutokea Mkoa wa Ruvuma 
 

Zamu ya Mratibu wa RUNECISO Juma Nyumayo ambayepia  ni Mmiliki wa Blog hii , Mhariri Msaidizi wa Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini (Tujifunze) na Reporter wa Redio uhuru FM kutokea Ruvuma 
Tour Guide Rasta Joseph Ndomondo akionyesha kisiwa cha miti ambacho sasa kimebaki mawe tu na miti michache kutokana na wavuvi kukata miti hiyo na kuathiri kabisa uoto wa asilli na kuleta mabadiliko ya tabia nchi ziwani humo. Bado kisiwa hicho kinaitwa kisiwa cha miti licha ya uharibifu huo ambao wananchi wa Liuli wamepanga kukabiliana nao kwa kuanzisha vikundi kazi katika kila kijiji na kuorodhesha wavuvi, wawindaji na wakata mbao wote ambao watapewa mafunzo ya kuvuna rasilimali hizo.
 

Bw Moses Konala aliyetangulia akimuangalia Tour Guide Rasta Joseph Ndomondo akimvuta Katibu Muhtasi wa RUNECISO Judith Lugoye na anayemfuatia Konala ni Charles Aidan wakitoka katika pango la Jiwe la Pomonda lenye uwezo wa kuhifadhi watu 100 hadi 200 kwa wakati mmoja wakati wa vita. Hivi sasa Pango hilo linatumika kwa wavuvi kujihifadhi wakati wa mvua, kutembelewa na watalii, kufanya sherehe na hata mapumziko.
 

Hilo ndiyo Jiwe la Pomonda kwa karibu linavyoonekana. Katika miamba ya jiwe hilo pia kuna miti yenye umri unaokadiriwa miaka 100-150 haikuwi wala haijawahi kukipita kisogo cha jiwe hilo maarufu la Pomonda
 

Safari ya Kurejea ufukwe wa Pomonda Raha Beach imeanza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiwe hilo la Pomonda. Hapo Bw. Nindi (Kulia) na Juma Nyumayo(Kushoto) wakiwa katika Boti, Utalii wa ndani ni muhimu kwa makundi mbalimbali ya watu ili kuhamasisha utunzaji wa vivutio kwa manufaa ya wananchi na wageni.
 

 

 


1 comment:

  1. SAFI SANA UTALII UFANYWE HUKO NYASA NZIMA ITABADILIKA

    ReplyDelete