Friday, June 7, 2013

HASSAN MAAJAR TRUST YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 320 KUSAIDIA ELIMU MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiandika kwenye daftari la mwananfunzi aliyekaa pembeni yake kama ishara ya matumizi ya madawati 320 yaliyokabidhiwa na taasisi ya Hassan Maajar Trust ya jijini Dar es Salaam tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense ikiwa ni jitihada za taasisi hiyo kusaidia elimu nchini.  Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilamu Serikali na huduma zilizopo badala ya kutoa mchango wowote. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga na Makamu Mwenyekiti Ndugu Shariff Maajar. Wa tatu kutoka kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
 
Wanafunzi wa shule ya msingi Kasense wakiwa wamekalia baadhi ya madawati yaliyotolewa shuleni hapo na taasisi ya Maajar Trust. Jumla ya shule nane (8) za Mkoa wa Rukwa kutoka kila Wilaya zenye upungufu mkubwa wa madawati zimepata madawati arobaini (40) kila moja kuondoa upungufu unaowakabili.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajr Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilaumu Serikali badala ya kusaidia katika huduma za jamii. Aliendelea kusema kuwa katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaboreka atakuwa dikteta kuhakikisha kila mtu wakiwemo wazazi wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaimarika. Kulia  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitoa taarifa fupi ya madawati kwa shule za msingi Mkoani Rukwa katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule hizo Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Aliishukuru taasisi hiyo na kusema kuwa Rukwa ina uhaba wa madawati 33,638 sawa na asilimia 50.2%.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense. Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuboresha mazingira ya kusomea watoto nchini Tanzania. Aliwaasa wadau wa elimu Mkoani Rukwa kuchangia katika sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga akisoma houtuba yake kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar shilingi laki moja na nusu ili aikabidhi kwa mwalimu mkuu shule ya msingi Kasense ikiwa ni sehemu ya azimio alilolianzisha na kuliita “Azimio la Kasense” KADARU (Kampeni ya Dawati Rukwa) katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipima uelewa wa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kasense Mkoani Rukwa kwa kuwapa mtihani wa kuandika wakati wa hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule hiyo, Kulia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.
Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Hassan Maajar Trsut Bw. Shariff Maajar, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa na Mkurugenzi Mtendaji Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga wakifurahia Ngonjera ya wanafunzi wa shule ya msingi Kasense katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati. 
Picha  ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wa taasisi ya Hasaan Maajar Trust.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview.blogspot.com

No comments:

Post a Comment