Wednesday, June 5, 2013

MSAFARA WA MANGWEA KUELEKEA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE MOROGORO

ZOEZI la kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya marehemu Albert Mangwea aliyefariki Dunia nchini Afrika Kusini Mei 28 umesitishwa huku umati mkubwa ukiwa haujamaliza kuuaga.

Kitendo cha Kamati ya maandalizi kukatisha zoezi la kuuaga mwili wa marehemu kwa sababu ya muda uliopangwa kukamilika iliwashangaza mamia ya watu waliokuwa kwenye foleni ya kusubiri kupata nafasi ya kutoa hesh
ma zao za mwisho mbele ya Jeneza la Mangwea.

Zoezi hilo liloanza saa 2:30 asubuhi imesitishwa saa 6:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, na msafara ukiongozwa na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwa katika Viwanja vya Leaders Club.

Barabarani Asakari wa Kikoso Cha Usalama Barabarani pia walijiapanga vizuri kuhakikisha kwamba msafara wa mwili wa marehemu unapita vizuri katika maeneo yaliokuwa yamepangwa kuelekea mjini Morogoro.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr Blue alifika katika viwanja hivyo akiwa amechelewa na kukosa muda wa kuuaga mwili wa Mangwea lakini alipokutana na mashabiki wa muziki wake aliweza kusimama na kuwapa pole.

Mwili wa Mangwea hivi sasa uko safarini kuelekea Mjini Morogoro ambapo utalala nyumbani kwa mama yake na kesho uwakazi wa Mji huo pia watapata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho. 

Endeleeni   kufuatilia taariza za mazishi ya Mangwea hapa hapa Habarimpya.com pia tunaomba maoni yetu kuhusu taarifa mbailmbali za Habarimpya.com

No comments:

Post a Comment