Friday, June 21, 2013

WANAVYOTUSEMA

Picture 
Katuni via/wavuti


Angalia wanavyotusema, hadi wanatuchora!
Na Juma Nyumayo, Songea
Hapa ni dhahiri hakuna umakini, "what is kubusti Blogu?" ukilinganisha na madhara ya kuua na kufufua?
Hakika kwa mtindo huu, hatutaaminika.

Kwa wote wanaoendesha Blogu na mitandao ya jamii tukianzia na wa mkoani Ruvuma, nchini Tanzania na kwingineko Ulimwenguni, naomba tuwe makini sana kuandika vitu vya ukweli ili kujenga Taswira njema na imani kwa wasomaji wetu.

 Blogu na mitandao mingine ya kijamii huwafikia watu wengi kwa haraka hivyo ina umuhim wa kuaminika kila kinachoandikwa.

Blogu ni chombo cha habari lazima kifuate Sheria, Kanuni na taratibu za Chombo cha habari kikiwa na sera zinazoeleweka kwa wasomaji wake. Ni muhimu kuhakikisha Blogu inachapisha na kutangaza vitu vyenye "Ukweli na Kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza."

Publish "The truth and try to minimize harm,". Haitakuwa na maana unachapisha na kutangaza ukweli unaoacha madhara makubwa kwa wasomaji wako na jamii husika. haina maana kabisa.
Mfano unaweka picha zenye muonjo mbaya 'bad taste' wasomaji wako wanaumizwa/ wanakerwa na picha hizo na kuwapa uwezo wa kuamua kutofungua tena Blogu yako.

Hasara hii ni kwa nani katika ulimwengu wa kuhabarishana? Maana yake hasara hii ingeweza kuzuiliwa kwa kufuata misingi ya Chombo cha habari katika maamuzi ya picha gani ichapishwe bila kuomba radhi na ile inayotakiwa ichapishwe kwa kuomba radhi na baadae kuondolewa.

Asante kwa katuni hiyo hapo juu, Inatukumbusha tukiwauwa wote, basi zamu yetu imefika, tujiue na tujifufue. Kumiliki Blogu isiwe sababu ya kuendekeza mabo ya kijinga na kuanza kujenga utamaduni ovyo ovyo. 

No comments:

Post a Comment