Kamanda Nsimeki na Meno ya Ndovu: Patachimbika Ruvuma
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki akipanga meno ya Ndovu kulingana na uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo.
Mwandishi wa habari Amoni Mtega akiwa amenyanyua jino la Ndovu
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya ndovu 18 yenye uzito wa kilo 84 yenye thamani ya Shilingi 216,000,000 sawa na dola 15 elfu za Kimarekani. Kwa meno hayo ni sawa sawa na Tembo tisa waliouwawa kikatili kisa kumiliki meno hayo yanayohitajika na majangiri wasio na huruma na viumbe hivyo vilivyobeba meno yenye thamani kubwa.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alisema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku katika Kijiji cha Majala Kata ya Nandembo wilayani Tunduru.
Kamanda Nsimeki, alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo lilitokea baada ya askari Polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa ambao kwa bahati mbaya hawakukamatwa.
Tukio hilo limekuwa la pili la katika kipindi kifupi lile la kwanza lilitokea katika kijiji cha Hanga wilayani Namtumbowsiki mbili zilizopita
Kamanda Nsimeki ametangaza kiama kwa majangiri mkoani Ruvuma na amewataka wajisalimishe la sivyo watakiona cha mtemakuni.
"jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama na hasa tembo" alisema Nsimeki.
Pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.
No comments:
Post a Comment