Thursday, June 6, 2013

IGP Said Mwema

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”

Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.

06
JUNI,
2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Said Mwema, amefanya mabadiliko ya makamanda na
wakuu wa upelelezi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Katika mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Michael Kamhanda amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Mungi ambae alikuwa
Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Aidha, DCP Ally Mlege aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa utawala na raslimali watu.

Vilevile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa
Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai  na nafasi yake inachukuliwa na
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha ACP Camilius Wambura.
Aidha, ACP Duwan Nyanda aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi anaenda kuwa Mkuu wa
Upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Arusha.

Uhamisho huo ni wakawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la
Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).

No comments:

Post a Comment