Thursday, June 27, 2013

DU SIKU ZA UTUMWA BAGAMOYO, WATUMISHI WA UCHAPAJI WIZARA YA ELIMU WATOA MACHOZI

 Mhariri Msaidizi wa Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini Bw. Juma Nyumayo (kulia) akishika pembe ya ndovu iliyobebwa na sanamu ya Mtumwa iliyojengwa mbele ya jingo mlango wa kuingilia Caravanserai. Hapo ni Hoteli ya wafanyabiashara wa masafa marefu ya watumwa ijulikanayo kama Caravanserai jengo lililopo katika mji wa kihistoria na maendeleo  ya kuanza kwa shule, huduma za afya na biashara za kila aina ikiwa ni pampja na biashara ya Utumwa hapa Tanganyika, (sasa Tanzania) na Afrika ya Mashariki. Picha hii imepigwa Jumatatu 24/6/2013 wakati watumishi wa Uchapaji, Vituo vya Uchapaji Kanda na Kituo cha Kisomo Mwanza ambao wapo chini ya Idara ya Elimu ya Watu Wazima, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walipotembelea maeneo ya Historia ya Mji huo kwa lengo la kujifunza uhifadhi wa majengo na historia ya maeneo hayo kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho hapa ulimwenguni. 

Mlango mmojawapo uliotengenezwa kwa ujuzi na wachongaji wasanii wa Enzi hizo uliotumika na wafanyabiashara wa kiarabu waliojihusisha na biashara ya utumwa huko Bagamoyo, Tanzania bila kushau maliasili ikiwa ni pampja na meno ya ndovu.

Hayo majengo ya Enzi hizo bado yapo, na hapo ni moja ya mtaa mashuhuri wa kibiashara katika Mji wa Bagamoyo (bonge ya Street) enzi hizo ambapo ni matajiri tu w biashara ya utumwa waliweza kumiliki majengo hayo na kurandaranda katika mitaa huku wakijipongeza kwa kunywa kahawa na kula  tende baada ya kufanikiwa kibiashara ambayo ilichukua masafa marefu kwa kuwauza binadamu ambao waliuzwa kama mihogo na kuilinganisha kwa ukubwa na ubora na wakati mwingine mfanyabiashara aliweza kupata nyongeza ya mtumwa mdogo dhaifu kama wafanyavyo kwenye ndizi endapo amemnunua mtumwa mwenye nguvu nyingi umbile kubwa kwa bei kubwa. Hapo baadhi ya kazi za sanaa za mikono kama kuchonga, kuchora , kufinyanga na nyinginezo zinauzwa kama unavyoziona katika picha hii sasa. 


Ni Mtaa mmojawapo wa kale hapo mjini Bagamoyo


Soko kuu la kale hapo Bagamoyo mpaka sasa linatumika kwa kuuza kazi za sanaa kwa watalii wa ndani na nje kama inavyoonekana

Ndani ya Jengo la Caravan sarai kuna makumbusho ambayo inaonesha picha mbalimbali za majengo ya kanisa misikiti ya utawala shule na wavumbuzi waliowahi kupita hapo Bagamoyo kama Dr Livingstone na wengine kibao. Hapo Mtumishi wa Kiwanda cha Uchapaji Press 'A' Lukia akiangalia picha hizoo ndani ya chumba cha makumbusho katika jengo la Caravanserai.
 

 

Mhariri wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye makao yake Makuu Mbeya, (kulia) akipiga picha kisima cha kale huku baadhi ya watumishi wakiangalia  na kusikiliza maelezo toka kwa kijana muongoza watalii hayupo pichani.
 
 
 
 
Kijana Muongoza watalii (aliyevaa T-shirt kushoto) akiwapa maelezo baadhi ya watumishi wa Uchapaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu kisima cha maji cha kale ambacho kinatumika mpaka leo ndani ya jingo la Caravanserai mjini Bagamoyo. Picha zifuatazo ni makundi mengine yakipewa pia maelezo kuhusu kisima hicho.
 

No comments:

Post a Comment