Na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amewavisha vyeo maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi 21 katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam. IGP Mwema aliwavisha maofisa hao vyeo hivyo baada ya kupandishwa na mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuanzia mei 28 mwaka huu.
Katika hafla hiyo, IGP Mwema aliwavisha maofisa wawili cheo cha Kamishina wa Polisi ambao walipandishwa kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) na kuwa kamishina wa Polisi(CP), maofisa hao ni aliyekuwa Naibu kamishina wa Polisi Suleimani kova na Naibu Kamishina wa Polisi Issaya Mngulu ambao sasa hivi wamepanda na kuwa makamishina wa Polisi.
Wengine 19, walivishwa vyeo vya Naibu Kamishina wa Polisi ambao nao pia walipandishwa kutoka cheo cha kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi na kuwa Naibu kamishina wa Polisi ni Pamoja na Mkuu wa utawala na rasilimali Naibu kamishina wa Polisi(DCP) Thobias Andengenye, Mkuu wa Opereheni Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Simon Sirro, DCP Brown Lekey, DCP Hamdani Omari Makame, DCP Kenneth Kasseke, DCP Sospeter Kondela, DCP Ernest Mangu, DCP Abdulrahman Kaniki, DCP Adrian Magayane, DCP Husseni Laisseri, na DCP Anthon Mwami.
Wengine kati yao ni DCP Mohamed Mpinga, DCP Mpinga Michael Gyumi, DCP Ally Mlege, DCP Hezron Gyimbi , DCP Jonas Mugendi na DCP Michael Kamuhanda ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa.
Miongoni mwa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi walipandishwa cheo cha Naibu kamishina wa Polisi, wapo maofisa wawili(2) wa kike ambao ni alikuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Bi. Adolfina Chialo ambaye sasa amepanda na kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) na aliyekuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Bi. Elice Mapunda naye pia amepanda na kuwa Naibu Kamishina wa Polisi(DCP).
Kwa upande wake Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Elice Mapunda alisema kuwa yeye ameshukuru sana kupata cheo hicho, kwani ni mara ya kwanza kwa mofisa wa kike wa Jeshi la Polisi kupata cheo hicho katika Jeshi la Polisi
IGP Mwema alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa rais na amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua mchango wa utendaji wa maofisa wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao,
Aliongeza kuwa “ Ni heshima kubwa sana kwa Jeshi la Polisi kusema kuwa amelijengea Jeshi mpanuko mkubwa kwani tangu tupate uhuru mwaka 1961 hatujawahi kupanua jeshi kwa kiwango hiki.
Aliwataka maofisa walipandishwa vyeo kuwa kioo na mfano katika kusimamia, kupanga na kutathimini kwa kuonyesha dira ili maofisa na askari wengine waweze kuiga katika kutoa huduma bora kwa ndani na nje.
No comments:
Post a Comment