Sunday, June 30, 2013

OBAMA ANASIMULIZI GANI KUHUSU AFRIKA?

Obama ana simulizi mbaya ya Afrika kichwani mwake

 
Imeandikwa, imewasilishwa na Maggid Mjengwa--

BARACK Obama ametua Afrika. Mguu wake wa kwanza ameukanyagia Senegal. Neno lake kuu akiwa Senegal ni DEMOKRASIA. Ameisifu Senegal kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kukuza demokrasia barani Afrika.

Kisha ametua Afrika Kusini. Jana Jumamosi ametembelea Kisiwa cha Robben, mahali ambapo Nelson Mandela alifungwa kwa miaka 27. Inahusu DEMOKRASIA. Bila shaka, Obama ataisifu Afrika Kusini kwa kukuza demokrasia yake na hivyo kuinua uchumi wake. Maana, pasipo na demokrasia ni nadra kwa uchumi kukua.

Kesho Barack Obama atatua Dar Es Salaam, Tanzania. Huhitaji kuwa mtabiri, kujua , kuwa Barack Obama atalitamka neno DEMOKRASIA akiwa Tanzania. Huenda Obama akaitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika kudumisha Amani na Umoja miongoni mwa watu wake. Lakini, bado Obama atasisitiza pia umuhimu wa demokrasia na uhuru zaidi wa vyombo vya habari barani Afrika.

Obama anaipenda Afrika, ni bara alilozaliwa baba yake mzazi, Dr. Barack Hussein Obama, Sir. Hivyo, kwa Barack Obama, Afrika ni bara la asili yake, na Kenya ndiko iliko asili yake. Ndiko liliko kaburi la baba yake.

Lakini, Obama ana simulizi mbaya juu ya bara hili.....

Soma zaidi: mjengwablog.com


Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment