Tuesday, June 11, 2013

SOKO KUU LA SONGEA MANISPAA LILIVYOKUTWA LEO JUMANNE


Ni Soko linalokuwezesha kupata kila kitu katika paa moja"..everthing under one roof" Soko Kuu la Songea hapo kuna Kinu, Koroboi, fagio, Mifuniko, nyungo, majiko ya mkaa na bidhaa nyingine za maandalizi ya jikoni.

 
Hali ya Chakula upokeaji bidhaa kwaajili ya chakula kwa wananchi wanaotegemea huduma toka  Soko Kuu la Songea  ni nzuri na bei zimepungua ikilinganishwa kabla na msimu wa mavuno ulioanza kwa aina mbalimbali ya chakula ikitanguliwa na mchele, ndizi, mahindi, maharage. baadhi ya vitoweo kama dagaa nyasa, samaki, na nyama imebakia vilevile leo. hapa angalia picha chache ilivyokuwa sokoni humo.

Hapa ushindwe wewe, Mahindi mekundu kwaajili ya Bisi, Ulezi, Mahindi ya kande, Karanga, Njugumawe, Njegere kavu, Mbaazi, Choroko... na aina zote za kundekunde

Viungo mbalimbali kwaajili ya chai, pilau na mapishi mengine. Viungo hivi husaidia pia kutengenezea dawa kwajili ya matibabu mbalimbali mbadala



Ndizi nazo ndio hizo


Usishangae kuwa hicho ni nini? huo ni udongo mweupe, mwekundu na uliotiwa viungo kwaajili ya akinamama.

 

1 comment: