Wednesday, June 5, 2013

HATIMA YA MGOGORO WA WACHINJA NYAMA ZA NG'OMBE NA MAAFISA WA MANISPAA YA SONGEA KESHO

Magari ya kubebea nyama toka machinjio ya Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma yakiwa yanapakia nyama kiasi kutokana na kuchinjwa ng'ombe wachache na kwa kuchelewa kufuatia wachinjaji na wanaouza ng'ombe kwa mdada kutangaza mgogoro wa kutotaka kuchinja ng'ombe kwaajili ya kuvunjiwa mazizi yao jana.

Mwenyekiti wa Wachinjaji Manispaa ya Songea, ambaye pia ni Diwani wa Misufini, mhe. salum Omari Mfamaji akiwaondoa wasiwasi wenye ng'ombe, wachinjaji na wategemezi wa shughuli za uchinjaji katika machinjio ya Msamala leo asubuhi baada ya kutangaza mgogoro jana na kudai wajengewe mazizi yao ndipo waendelee kutoa huduma hiyo.

Afisa Mifugo wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Ramadhani Mwaiganju, (wa tatu toka kushoto) akihojiwa na waandishi mara baada ya kufika katika machinjio hayo asubuhi ya leo ili kutoa ushauri kwa pande zote zilizohusika na mgogoro huo.

Wateja wa Utumbo, Makongoro, damu maarufu kama "Ubende" kwa Kingoni na huduma nyingine wakiwa wamezuiliwa lango kuu la kuingilia kufuatia mgogoro huo uliotangazwa jana usiku wa kutochinja ng'ombe kisa ikikwa ni kuvunjiwa mazizi yao bila taarifa.


Sehemu ya nyama ya ng'ombe wachache waliochinjwa kwa kuchelewa leo ikiwa ni juhudi za Mwenyekiti wa wachinjaji, Mhe. Salum Mfamaji na Diwani wa kata ya Msamala Mhe. Sharif Mgwasa (Kulabest) ambaye ameahidi kuhamishia Ofisi yake hapo hadi kuumaliza mgogoro huo ambao umeonyesha kuwepo hapo kwa chinichini kwa muda mrefu hadi ulipolipuka jana baada ya maafisa wa afya ya mifugo wa manispaa ya Songea kuvunja maziziz ya kuhifadhia ng'ombe kwa kutaka wahame eneo hilo.


























No comments:

Post a Comment