Tuesday, June 18, 2013

TGNP NA KITUO CHA SAUTI ZA JAMII SONGEA



Afisa Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Lilian Kitunga, akimkabidhi Vifaa vya  Mawasiliano Kompyuta, Printer, Moderm na muda  wa Maongezi wa  Shilingi 500,000/= Mwenyekiti wa Kituo cha Sauti ya Jamii, cha Taarifa na Maarifa Songea   Fatuma Misango.

Mama Siwajibu Gama, akisisitiza jambo kwenye kikao cha  Wanachama wa  Kituo cha  Sauti ya Jamii,Taarifa na Maarifa Songea

Wanaharakati wakiwa pamoja na mwandishi wa habari, Nathan Mtega (wakwanza kushoto) wakisikiliza maelezo ndani ya  Ofisi za Sauti ya Jamii, Kituo cha Taarifa na Maarifa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Ijumaa Juni 13, 2013.

Kutoka kushoto ni Wanaharakati Jane Kasian , na Mama Karimu wakisikiliza kwa makini makabidhiano ya Vifaa kutoka TGNP Juni 13, 2013 vitakavyosaidia kupaza sauti za wanawake waliopo pembezoni.

IKIWA TAARIFA ndiyo nguvu ya kupambana na kusaidia wanawake waliopo pembezoni, Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP imeendelea na harakati zake za kusukuma mbele gurudumu la ukombozi kwa wanawake walioko pembezoni.
 
Wilayani songea mkoa wa Ruvuma  tayari TGNP imewapiga jeki wanawake hao katika kituio chao cha Sauti ya jamii, Taaarifa na Maarifa kwenda kidigitali kwa kutoa msaada wa vifaa na muda wa kwenda hewani.
 
TGNP kupitia Ofisa wake wa mawasiliano, Lilian Kitunga, amekabidhi vifaa Mawasiliano  ambavyo ni Kompyuta, Printer, Moderm na muda  wa Maongezi wa  Shilingi 500,000/=.
 
  Mwenyekiti wa Kituo cha Sauti ya Jamii, cha Taarifa na Maarifa Songea  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa sharia (SOPCE)  Fatuma Misango, ameshukuru kwa msaada huo kuwa umetolewa kwa wakati na ni ukombozi kwa wanawake si wa Songea tu bali kwa mkoa mzima.

  

 Naye Jeni Kasian alisema kuwa   katika kutetea  haki  ni vyema kuunganisha nguvu toka mtu mmojammoja na makundi.
 " idadi kubwa ya wanaonyanyaswa ni wanawake na watoto hivyo kuna kila  sababu ya kuwa na sauti ya pamoja ili kukabiliana na vitendo vya kikatili na unyanyasaji," alisema.
  

Amebainisha kuwa, matukio mengi ya unyanyasaji wa kijinsia yanayofanywa dhidi ya wanawake na watoto huku waathirika wakiwa hawajui waelekeze wapi kilio chao sasa kimepata ufumbuzi.
Aidha, alisema jane kuwa kuwepo kwa Kituo hicho cha msaada wa kisheria kikiwa na vifaa vya kurahisisha mawasiliano, upashanaji wa taarifa na kupata habari kwa haraka itakuwa ni ukombozi kwa watoto na wanawake na kuwaweka katika mazingira bora ya kupata maendeleo.
 

 Ofisa toka TGNP Lilian  Kitunga amesema madhumuni ya kugawa vifaa hivyo ni  kuwasaidia wanawake walio wengi ambao wako pembezoni na kwamba imebainika uwezo wao wa kupata habari mbalimbali ni mdogo.
 

Mwisho.

No comments:

Post a Comment