Friday, April 19, 2013

WASIWASI WA MAISHA BAADA YA MLIPUKOMASHINDANO YA MARATHON BOSTON MAREKANI


Nimeamshwa na simu kutoka Emergency Alert ya mji wa Cambridge, MA wakisema kuwa ni marufuku kutoka nje ya majumba yetu leo! Hakuna usafiri, wameomba sehemu za kazi zisifungue!

Wanasema kuwa hakuna kufungua mlango hata kama ni polisi, wanasema kuwa jamaa anataka kuua watu!

Jana usiku ilikuwa balaa hapa Cambridge! Cambridge ni nje ya Boston.  Kwanza kwenye saa tatu na nusu (9:30PM) tulisikia kuwa majambazi walivamia duka la  7-11 Central Square!

Kukaa kidogo tukasikia Polisi kapigwa risasi Chuo Kikuu cha MIT! Baada ya muda mfupi wakasema yule polisi kafa!

Kwenye saa tano tukasikia mtu kaibiwa gari yake aina ya Mercedes Benz, kwenye kituo cha mafuta!  Ni mwendo mfupi toka ninapokaa! Nikaanza kusikia milio ya gari ya polisi!

Kumbe polisi wa kila aina walikuwa wanawafukuza  karibu na Arsenal Mall. Milio ya risasi balaa, ambulance na magari ya polisi yalikuwa yanafukuzana, kwenye TV, tukaona kila mtu aliyefanana na Mspanish, Mwarabu kasimamishwa na kusachiwa!

Sikulala hadi saa nane na nusu! Nimeamshwa na simu ya Emergeny Alert!


Source: http://www.wavuti.com/

No comments:

Post a Comment