Friday, April 12, 2013

Asante Dkt. Matomola kwa kuanzisha na kuiendeleza KIUMA inayoleta taswira ya maendeleo Kusini


Mafundi na Wanafunzi wa Makenika katika workshop ya KIUMA iliyopo Milonde Matemanga  zaidi ya maili 45 toka Tunduru mjini. Workshop hiyo ni msaada mkubwa kwa watumiaji wa Mitambo wa eneo hilo ambalo sasa kunajengwa barabara kiwango cha lami japo inasuasua.


Aliyefunga Kilemba ni Mrs Nyumayo akiwasiliana na wanawe wakati akijulishwa ubovu wa gari lake na Mwanafunzi wa makenika KIUMA aliyejulikana kwa jina moja tu, Dan ambao walimsaidia  kwa ushauri na kulitengeneza gari hilo.


KIUMA Workshop inavyoonekana

Afisa Elimu wa Wilaya Mstaafu aliyewahi kufanya kazi maeneo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na Wilaya za Mbinga, Tunduru na Liwale Bibi Rachel Makochela akifurahi kukutana na Mwandishi wa habari wa Nipashe Mkoani Ruvuma Bw. Gideon Mwakanosya, walipomtembelea anakofanya kazi sasa Kituo cha Ufundi na Maendeleo (KIUMA) kilichoanzishwa na Dkt. Matomola Matomola.


Mrs Hindu Juma Nyumayo (Kushoto) akiwa na Afisa Elimu Mstaafu, Bibi Rachel Makochela, akifurahia mazingira ya eneo la KIUMAalivyotunzwa hasa kuona miti ya kienyeji iliyoachwa bila kukatwa na  majengo kama nyumba, madarasa, mabweni na wodi zikiwa chini ya miti hiyo.
Bibi Rachel Makochela aliishi vyema na Mrs Nyumayo wakati akiwa Afisaelimu wilaya ya Tunduru na mumewe akiwa Afisa msaidizi wake.
Na Juma Nyumayo, aliyetembelea KIUMA- TUNDURU

KIUMA ni jina ambalo hivi sasa linatikisa katika mioyo ya wakazi wengi kusini mwa nchi ya Tanzania.
Mika 15 iliyopita ungelitamka jina la kiuma usingelieleweka unaqsema nini.
KIUMA ni Kituo cha Ufundi na Maendeleo kilichoanzishwa na Dkt Mzalendo ajulikanae kwa jina la Dkt Matomola Matomola.
Nadiliki kumuita mzalendo kwakuwa nilishawahi kuhojiana naye na kufanya nae kazi moja  ya kuwatafuta na kuwaendelezsa vijana katika masomo ya sayansi ili wajiunge katika Kituo hicho.
Nikiwa wakati huo kama Katibu  wa Shirikatuliloliita Tunduru Academic Forum (TAF) niliwahi kumuammbia Dkt Matomola mbele ya vijana zaidi ya 150 ambao walikuja kusikiliza mkutano wetu katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Frank Weston kuwa Dkt Matomola ni Mzalendo kwakuwa ameamua kuwekeza katika maendeleo ya watu hukohuko mashambani na hasa kusini mwa Tanzania. Nilimuambia watu kadhaa wamewekeza katika Glosary, Saloon n.k. na kwamba kwa mtaji alionao angeliweza kuwekeza mahoteli ya kifahari huko Dar au Mtwara na kuvuna pesa nyingi.
Tuache hayo.
Kiuma imejengwa Mashamabani, lakinini sasa imebadilika.
KIUMA Kuna Kanisa kubwa kwaajili ya kuwalea watu wa imani tofauti kiroho, Kuna Hospitali kubwa inayotoa matibabu pia upasuaji mkubwa, kuna shule za Ufundi wa aina zote kuanzia uashi, useremala, magari, umeme nk.
KIUMA ina Sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi sita. Kuna kituo cha kilimo, Chuo cha Uuguzi , Ualimu vinavyombatana na hivyo na kusababisha kukua kibiashara kwa kasi ya ajabu chini ya miaka 12 hivi.
KIUMA kwa mawasiliano ipo barabarani ukitokea wilaya ya namtumbo mkoani Ruvuma kuelekea Tunduru na ina Uwanja wa Ndege unaojitegemea. 
KIUMA sasa ni mkombozi kwa wanataaluma mbalmbali wanaostaafu na wale wenye sifa nzuri. Wengi wa walimu, madaktari, watawala, wachumi na wenye fani nyingine wameajiriwa na KIUMA ili kuendeleza ujuzi wao kwa kizazi cha wananchi hasa wale waliotengwa kwa kipindi kirefu kutokana na mila na mazingira magumu ya watu wa wilaya ya Tunduru na za Kusini kwa ujumla.
Hivi sasa KIUMA imekuwa ni kivutio cha wapenda maendeleo kuwapeleka watoto wao kujifunza Nyanja mbalimbali.
Nadiriki kuandika kwa herufi kubwa ASANTE DKT. MATOMOLA kwa ndoto zako zimekuwa kweli.  Hukutaka ufaidi peke yako. Ulitaka ushiriki na wananchi wa pembezoni, waliokuwa wakipoteza maisha kwaajili ya uzazi kwa kukosa huduma bora za afya na upasuaji. Ulianza kwa mafiga matatu ya Elimu ya Ufundi, AFYA, KILIMO sasa yameongezeka saaana.
Dkt Matomola amedhihirisha kuwa yeye ni msomi anayeweza kuleta mabadiliko. Yafaa aigwe.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment