Bw Ernest Sungura (kulia) na Juma Nyumayo
Na Juma Nyumayo, Songea
Uongozi wa Tanzania Media Fund(TMF), umetembelea Mkoa wa Ruvuma kuona maendeleo ya tasnia ya habari na changamoto zake.
Mkurugenzi wa Mfuko huo, Bw Ernest Sungura na Afisa anayeshughulikia Ruzuku za mashirika, Bw Alex walikua na ziara ya mkoani hapa kwaq shughuli za kikazi ambapo walipata fursa ya kutembelea asasi, vituo vya habari na kuzungumza na wadau mbalimbali.
Bw Sungura alisema walitembelea radio Jogoo FM, Ruvuma Press Club pia kuongea na wadau mbalimbali wakiwemo wale waliowahi kupata ruzuku toka mfuko huo.
Waandishi wa awali waliopata ruzuku toka mfuko huo wa TMF ili kufanya kazi zahabari za kiuchunguzi wa kina kuhusu sekta mbalimbali mkoani hapa, ni pamoja na Adam Nindi, Juma Nyumayo, Joyce Joliga, Thomas Lipuka Komba, Albano Midelo na engine kadhaa walioweza kufanya vyema kutumia fursa ya mfuko huo.
Katika Mazungumzo yao na waandishi waandamizi mkoani Ruvuma ambao walimtembelea katika Hoteli ya Herritage Cottage, Bw. Sungura ameendelea kusisitiza umuhimu wa waandishi kuandika habari zitakazochochea maendeleo, mshikamano wa watanzania na kuleta amani na utambulisho wa Taifa katika Nyanja za kiamtaifa.
Awali, Mwandishi Mwandamizi Bw. Adam Nindi, aliushukuru utendaji wa TMF kwa kuwajali waandishi wa pembezoni kuibua masuala (Issues) ambayo ni kikwazo kwa maendeleo ya wananchi kama changamoto zinazowakabili wananchi hao katika masuala ya Ulinzi na Usalama wa mali zao, afya, Elimu, kilimo, uchumi na mambo mengine ya kisiasa na kijamii. " Sisi tunawashukuru TMF kutujengea uwezo wa kufanya kazi kwa kujiamini kwaajili ya watanzania," alisema Bw. Nindi.
Kiongozi huyo amerejea jijini Dar es Salaam leo. |
No comments:
Post a Comment