Na Juma Nyumayo, Songea
Nimekuwa Msomaji mzuri wa Blogu ya Prof. Joseph Mbele.
Makala nyingi anazoandika, picha anazopost na mazungumzo yake anasisitiza sana watu kuelimika. watu wajifunze mila na desturi mbalimbali kwa maendeleo yao.
Prof. Mbele husafiri na wanafunzi wake (Wamarekani) kuja nao nchini na kutembelea maeneo mbalimbali. Wanajifunza kwa vitendo. Mimi licha yakuwa Mwandishi wa habari kitaaluma, ni mwalimu pia.
Tumesisitizwa na wataalamu wa elimu (Walimu wetu) na tunaendelea kusisitiza ili kujifunza vyema na kujenga kumbukumbu ya kudumu, elimu kwa vitendo itumike zaidi kuliko nadharia. Vitendo vinahusisha milango mingi zaidi ya fahamu.
Prof. Mbele katika Blogu yake ya hapakwetu.blogspot.com anafundisha mengi, nimeona jinsi anavyotembelea maonesho hakosi kupiga picha mabanda yanayoonesha vitabu. Katika Blogu yake anaonyesha machapisho mbalimbali na vitabu vipya.
Kulikoni Prof. Mbele kupendelea zaidi vitabu, kunani kwenye vitabu. Tabia iliyoibuka ya baadhi ya watanzania kujiingiza kwenye mijadala mizito wakati wao ni 'weupe'. Weupe kwakuwa hawana hazina kichwani iliyotokana na kusoma vitabu vya mijadala husika. Inapotosha watu na nchi kwa ujumla.
Hapa nitaweka baadhi ya kazi zake chache. Hajaniruhusu lakini natanguliza kuomba radhi.
Hii ni kwa manufaa ya wasomaji wetu waweze kutembelea Blogu ya hapakwetu.blogspot.com kuchota maarifa.
Angalia kazi hizo, na uingie mwenyewe mtandaoni uone Falsafa yake. Kweli Prof. Mbele ni Mwalimu wa watu, kwaajili ya maendeleo ya watu na ulimwengu kwa ujumla.

Asante sana kwa kuweka taarifa zangu hapa kwenye blogu yetu pendwa. Mimi ni msomaji makini wa blogu hii.
ReplyDeleteNashukuru kwa uamuzi wako, kwani unanisaidia mimi ambaye ni mwalimu, kusambaza kwa walimwengu yale ninayoandika. Ndio wajibu wa ualimu, na narudia tena shukrani zangu kwako.
Asante saana Prof.Mbele. Tupo pamoja. Maaandishi yako na Maelekezo unayoyatoa ni hazina kubwa. Tutaendelea kufuatilia katika Blogu ya hapakwetu.blogspot.com kuchota hazina hiyo kwa maendeleo yetu. Asante kwa yote.
Delete