Na
Steven Augustino, Tunduru
MKAZI
wa Kijiji cha Daraja mbili katika kata ya Namwinyu Tarafa ya Matemanga Wilaya
ya Tunduru Mkoani Ruvuma ameuawa na tembo.
Mkazi
huyo aliyefahamika kwa jina la
Chalamanda Masapi (65) amefariki dunia baada ya kuvamiwa ghafla na
kushambuliwa na Tembo ambaye alikuwa na mtoto wakati akikagua uhalibifu wa mazao uliofanywa
na kundi la wanayama hao katika shamba lake lililopo nje kidogo ya kijiji hicho.
Mtoto
wa Marehemu Chalamanda, Rashidi Chalamanda ambaye alikuwa ni miongoni mwa
Shuhuda wa tukio hilo, alisema kuwa yeye na marehemu babayake
wakishirikiana na kundi la wananchi wanaolima katika eneo hilo walikwenda
katika mashamba yao kushiriki katika zoezi la kuwafukuza tembo hao ambao pia
walivamia Kijijini hapo na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao yao.
Alisema
katika tukio hilo la kushitukiza marehemu alijikuta akiwa mikononi mwa
mnyama huyo ambaye hakuwa hana hata chembe moja ya huruma ambaye baada ya
kumkamata kwa kutumia mkonga wake alimrusha juu na kumpiga katika mti
uliokuwa karibu na eneo hilo kabla ya kumkanyaga na kumsaga na baadae kumpiga
kwa kutumia Pembe zake na kumtoboa toboa vibaya mbavuni na tumboni.
Katibu
uchumi wa CCM Wilaya ya Tunduru, Bw.Yasini Masapi, akizungumzia hali na
mwonekano wa mwili wa marehemu Chalamanda alisema kuwa ama kweli mnyama
huyo alimpania kumtoa uhai kwani pamoja na kumtoboa kwa kutumia pembe hizo pia
Tembo huyo alimparua na kumkanyaga kanyaga na kuuvuruga kabisa mwili kiasi cha
kutomtambka kabisa .
Afisa
Wanyama pori wa Wilaya hiyo Bw. Peter Mtani, amekiri kuwepo kwa tukio hilo. Amesema kuwa tayari
idara yake imepeleka askari wenye silaha ili waende kuandaa mtego ambao utafanikisha
kuuawa kwa Tembo huyo.
Bw.
Mtani, aliendelea kueleza kuwa matukio ya Tembo hao kuvamia na kifanya
uharibifu katika mashamba ya wakulima wa Wilaya hiyo yamekuwa yakijitokeza mara
kwa mara na kwamba kutokana na hali hiyo idara yake imekuwa ikifanya kazi ya
ziada kuwafukuza wanyama hao ili wasiendelee kuharibu mazao ya watu.
Alisema
pindi inapo bainika kuwa Tembo hao wanazidi kufanya mashambulizi ya kuzulu
mwili ama kufanya mauaji kama ilivyo tokea idara hiyo pia imekuwa ikichukua
hatua za kuwasakaa na kuwaua tembo hao haraka iwezekanavyo ili wasiendelee
kusababisha madhara kwa watu wengine.
Akizungumzia
hali na muonekano wa mwili wa marehemu huyo Mganga katika hospitali hiyo
Dk. Gearge Chiwangu, alisema kuwa Marehemu alifariki dunia kutokana na kutokwa
na damu nyingi zilizo sababishwa na kutobolewa matundu manne ubavuni na tumboni
mwake.
Dk.
Chiwangu aliendelea kueleza kuwa sambamba na hali hiyo pia mwili wa
marehemu ulikutwa ukiwa umevurugika vibaya huku shingo yake ikiwa imevunjika na
kichwa kupasuka hali ambayo onesha kuwa hata kama asingefariki katika eneo la
tukio uwezekano wa kumsaidia kuokoa maisha yake usinge kuwepo.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusidedit Nsimeki, amethibitisha kuwepo kwa
tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili
kujiridhisha chanzo cha kifo hicho.
Mwisho
No comments:
Post a Comment