Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma, Bw. Mohamed A. Maje (Picha na Juma Nyumayo) |
WILAYA ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambayo ina maeneo ya kutosha kuwekeza katika Nyanja za Kilimo, Madini, Huduma za elimu, Afya, Sayansi na Teknolojia ya habari pamoja na mambo kadhaa ya kimaendeleo bila kusahau biashara za mawasiliano na uchukuzi sasa ipo vizuri kuwapokea wawekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo wa Wilaya hiyo, Bw Mohamed Maje, ameuambia mtandao huu jioni hii mjini Songea kuwa Namtumbo sasa ipo vizuri.
"Sasa umeme unakamilika hivyo watu waje wawekeze katika Nyanja mbalimbali," alisema Bw Maje pichani hapo juu.
Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu umeonyesha kuwa licha ya uwekezaji mkubwa unaohitajika katika kilimo, bado eneo la ujenzi wa nyumba za kuishi na majengo ya kupangisha biashara mbalimbali yanahitajika mjini Namtumbo, mji unaokuwa kwa kasi uliopo umbali wa Maili 40 toka makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma Songea.
Hivi sasa Wilaya ya Namtumbo inafahamika kimataifa kutokna na kukamilika kwa utafiti wa Madini ya URANI (Uranium) ambayo ni mengi na habari zilizopatikana vibali vimetolewa ili kuruhusu kuchimba madini hayo ambayo yatavutia wawekezaji wa kitaifa na kimataifa na kupatikana kwa ajira ya wasomi na watu wa kawaida.
Namtumbo sasa ipo katika ramani ya Dunia inayoonesha kuwa na madini muhimu katika kutengenezea vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nguvu za Nuklia pia kujenga vinu vya kuzalisha umeme.
No comments:
Post a Comment