Watoto wafuzu masomo bila wazazi kujua na wafungua milango kwa kutumia makalio
Na Steven
Augustino, Tunduru
WAZEE wa
tano kutoka katika Kijiji cha Mtonya, Wilaya Tunduru Mkoani Ruvuma wamezuiliwa
katika Kituo kidogo cha Polisi Nakapanya ili kulinda usalama wa maisha yao na
kuwafanya wasishambuliwe kutokana na kutuhumiwa kufanya ushirikina na
kuwafundisha taaluma hiyo watoto wawatu bila ridhaa ya wazazi wao.
Tukio hilo la aina yake,
lilitokea baada ya wazee hao wanaodaiwa kuwa na uwezo wa kufungua na kuingia
katika nyumba za watu kwa njia za mazingara kufumwa wakifanya vitendo hivyo
katika kijiji cha Mindu Wilayani Tunduru.
Taarifa
zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Nakapanya, Bw. Kubodola
Ambali, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Spia Msusa (50), Ayana Iddi (75)
Adresia Maulidi(68), Jenifa Saimon (60) na mwingine aliyefahamika kwa jina la
Binti Nyoya (60).
Bw. Ambali,
aliendelea kufafanua kuwa Mpango huo uligundulika baada ya wazazi wa Mtoto Ally
Milongo, kuamka na kuanza kumtafuta mtoto wao huyo mwenye umri wa miaka 10
kutoweka usiku wa manane ndani ya nyumba yao katika mazingira ya kutatanisha .
Baba wa Mtoto
huyo Bw. Milongo Ally, alisema kuwa baada ya tukio hilo la kutoweka kwa mtoto wao
yeye na mkewe waliamka na kuanza kumtafuta katika maeneo tofauti ya kijiji
hicho ambapo wakafanikiwa kuwaona Wazee hao wakiwa uchi wa mnyama pamoja
na kijana wao na walipojaribu kuwasogelea vikongwe hao walitoweka katika
mazingira ya kutatanisha.
Alisema baada
ya tukio hilo walimkamata mtoto wao na kwenda naye nyumbani kwao na baada ya
kumbana na kumtaka aeleze aliko kuwa ndipo akawataja watu hao ambao baada ya
kuitwa walikiri na kuomba radhi kuwa hawatarudia kumchukua mtoto huyo ambaye
walidai kuwa ni miongoni mwa washirika wao wa muda mrefu ambao tayari wameshampatia mafunzo ya kutosha.
Alisema
katika tukio hilo wazee hao walitozwa faini ya Shilingi 100,000 ambayo
waliilipa papo hapo na baadae wakaruhusiwa kuondoka kituoni hapo baada ya kundi
la watu waliojitokeza kuwaangalia kuondoka.
Akiongelea
tukio hilo Mtoto Ally Milongo, alisema kuwa mara kwa mara watu hao
wamekuwa wakienda kumchukua yeye na watoto wenzake wanne na kuwapeleka katika
maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwafundisha utaalamu kuingia na kuwachezea watu
na baadae hurejea majumbani mwao na kufungua milango kwa kutumia matako huku
wazazi wao wakiwa hawafahamu kinachoendelea.
Mwisho
No comments:
Post a Comment