Monday, April 15, 2013

UDP YAKOROMEA VIONGOZI WA SERIKALI

Na Steven Augustino, Tunduru

KATIBU Mwenezi wa UDP Taifa Bw. Simbili Makanyaga,  amewataka Viongozi
wa serikali na Waliopewa mamlaka na Wananchi kwa kuwachagua kushika
nyadhifa za Ubunge na Udiwani kutimiza wajibu wao katika kusimamia
miradi inayotolewa na serikali ili kurejesha imani kwa wananchi ambao
kwa sasa wameanza kukosa imani na utendaji wao.

Bw. Makanyaga,  ambaye yupo Wilayani Tunduru kwa ajili ya ziara ya
kikazi alitoa wito huo wakati akiongea na wananchi kupitia mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanja vya Balaza la Idd mji Tumduru
Mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa kama wamechoka kuwatumikia wananchi
kupitia dhamana walizo pewa ina faa waachie ngazi na kupisha watu
wengine tofauti na sasa ambapo wamekuwa wanakula mishahara ya bure.

Katika hutuba yake Bw. Simbili alitolea mfano Wataalamu wa idara za
afya na wahandisi wa idara ya Ujenzi Wilayani humo kuwa hivi sasa
hawawajibiki katika majukumu yao ya kazi hali ambayo imesababisha
miundombinu ya Barabara mjini humo kubomoka huku wahusioka wakiwa
hawaoneshi juhudi zozote kuziokoa.

Alisema kutokana na kuto wajibika kwao Barabara zote za mji huo katika
na kuwafanya watu kuru enzi za ujima kutokana na kuanza kubeba
wagonjwa kwa njia ya machela kutokana na magari na vyombo vingine vya
moto kushindwa kupita katika mitaa ya mji huo.

“hivi Wahandisi wa Ujenzi na wahusika wengine hamuoni aibu, hivi sasa
mji unanuka kutokana na mitaa yote kuwekwa mapumba ya mpunga
Barabarani zikiwa ni juhudi za wananchi kuzinusuru barabara zao na
kuwawezesha kupita” alisema Bw. Simbili ba kuwataka waisaidie Serikali
kwa kuiondolea lawama na matusi yasiyo kuwa na ulazima wowowte.
Kuhusu Idara ya afya Simbili alisema kuwa mbali na kuwepo kwa
malalamiko mengi ya kukosekana kwa huduma za uhakika kwa wananchi
lakini Wataalamu hao hivi sasa hawawajibiki kabisa hata kuagiza Madawa
na kuyaweka katika hospitali,Vituo vya afya na zahanati zote za
serikali.

Maeneo mengine yaliyoguswa katika hptuba ya kiongozi huyo ni pamaja na
maeneo ya Standi Kuu ya mabasi ambapo ndi uso wa Miji wa Tunduru eneo
ambalo hivi sasa ni chafu kupindukia lakini wahusika wanaonekana
kutochukua hatua zozote kuyatatua matatizo hayo.

Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Chande Nalicho pamoja
na kukiri kuwepo kwa hali hiyo alisema kuwa tayali ofisi yake kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
wamechukua hatua ya kuzifunga baadhi ya Barabara za miji huo kwa
maelekezo ya kuanza kuzifanyia ukarabati baada ya mvua kuisha.

No comments:

Post a Comment