Sunday, October 31, 2010

Tunaendelea hivi Oktoba 31, 2010
















PILIKA ZA UCHAGUZI OKTOBA 31, 2010

Dr. Emmanuel Nchimbi mgombea Ubunge Jimbo la Songea Mjini, akipiga kura yake leo saa 1:00 Asubuhi Kituo cha Kupigia Kura- Mateka Manispaa ya Songea kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Kituo hicho, Gerwada Kapinga akitoa maelekezo.
Baadhi ya wapiga kura katika Kituo cha Shule ya Luhira Kata ya Mshangano, wakiwa katika Mstari wakisubiri kuingia kupiga Kura. Wakati huo huo Waandishi wa Habari wakitoa matangazo ya Mojakwamoja, Mwenye Suti ni Riporter wa Star TV na Redio Free Africa mkoani Ruvuma, Bw. Adam Mzuza Nindi na anayepiga picha hiyo ni Mpenda Mvula ambapo aliyepachika Camera begani akiwa katika mstari ni Muhidin Amri wa Majira.


Hiyo ni jana wakati kampeni za CCM siku ya mwisho kule Kiburang'oma Lizaboni, Manispaa ya Songea zikiwa zinafungwa rasmi, hapo juu na chini wapambe wakiwa makini kusikiliza sera na midundo ya muziki wa kizazi kipya kuipamba CCM na wagombea wake.














Foleni ya wapiga Kura bila kujali mwanamke au mwanaume eneo la Makumbusho ya Mashujaa ya Vita vya Majimaji Mahenge manispaa ya Songea leo saa 1:15 Asubuhi watu wameitika si mchezo.





Bw. Adam Mzuza Nindi, kwenye Kituo chake cha kupigia Kura Mjimwema Manispaa ya Songea akipokea maelekezo baada ya kukabidhi kitambulisho chake cha kupigia Kura leo majira ya Saa 5:45.










Friday, October 29, 2010

Haya Dr Nchimbi na kampeni za mwishomwisho

Dr. Emanuel Nchimbi anayepungia mkono wananchi mara baada ya kuhutubia mkutano wake katika kata ya Bombambili Mtaa wa Miembeni akisindikizwa kwa maandamano makubwa yanayoashiria kuungwa mkono kwa CCm. Kata hiyo inakabiliwa na upinzani toka Chadema katiak kiti cha Udiwani ambapo mgombea wake Ken Moto anamtikisa mgombe toka CCM ambaye alikuwa Diwani awamu iliyopita Golden Sanga.
Mtoto huyo hapo juu jina lake halikuweza kufahamika mara moja akiangalia manjonjo ya Dr Nchimbi kumuombea Kura mgombea Udiwani Kata ya Bombambili Manispaa ya Songea Golden Sanga maarufu Sanga One wote ( awapo Pichani) chini toka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Muhidin Amri na Katibu wa Mbunge huyo Andrew Chatwanga na dereva wao Jogoo eneo la Mjimwema Manispaa ya Songea
Sasa Kazi, Vijana wa IGP Mwema chini ya usimamizi wa Kamanda wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda wakifuatilia matukio na kulinda usalama wa raia katika mikutano ya mwisho ya kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 31, 2010 Siku ya Jumapili, hapa wakivinjari viwanja vya Samora kule kata ya Mjimwema Manispaa ya Songea.



Mkurugenzi wa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula nchini, Charles Walwa akistaajabu mahindi yaliyopo nje katika Ghala la wakala huyo lililopo Ruhuwiko Mjini Songea. Mkurugenzi huyo ametangaza nguvu nyingi kuelekezwa vijijini na kuwahakikishia wakulima na wafanyabiashara kununua kiasi chote cha mahindi hata baada ya Uchaguzi. hadi juzi tani 30,000 zimenunuliwa mkoani hapa na kiasi cha tani 20,000 zitanunuliwa kwa mpango mzuri zaidi.



Thursday, October 21, 2010

Siku kenda kuelekea Uchaguzi mkuu! Songea ipo hivi

Hiyo Ramani ya Tanzania, Jimbo la Songea Mjini lipo hapo kwenye mji wa Songea. Wananchi wengi mjini hapa wanamtakia mafanikio na heri katika uchaguzi Mkuu, Mgombea wa CCm Dkt Jakaya M. Kikwete na Ubunge wanategemea atapeta kwa kura nyingi Dkt Emmanuel Nchimbi na kukalia kiti hicho kwa miaka mingine mitano, hayo ni ya Songea.
Hapa Dkt Jakaya Kikwete (Kushoto) akimsalimia Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima nchini, Salum Mnjagila, alipotua Uwanja wa ndege wa Songea, mwishoni mwa mwaka 2009.

Hapa chini Dkt Emmanuel Nchimbi akifurahia jambo mara baada ya kukabidhi Majengo ya Shule ya Sekondari Mkuzo mwaka huu. Aliyevaa joho ni Aliyekuwa Meya wa manispaa ya Songea Mhe. Gerald Ndimbo ambaye sasa anatetea kiti chake cha udiwani Kata ya Ruhuwiko na anayefuatia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini, Hemedi Dizumba Luambano na kule nyuma ni madiwani awamu iliyopita. Wengi waliopita kwenye kura za maoni CCM.


Wednesday, October 20, 2010

Peramiho na Mlale JKT, wengi mtakumbuka!


Kanisa la Peramiho na minara yake yote miwili hapo juu. Angalia huo mnara wa kulia na saa inayozidi miaka 100 bila kurekebishwa na haijapoteza Majira. Na hiyo picha nyingine chini, inaonyesha kanisa hilo la Peramiho ubavuni ukitokea Trade School upande wa Magharibi na kuelekea Hospitali na ni pale kwenye Mzunguko (Round Obout) Pameboreshwa kwa lami toka pacha ya Mbinga hadi Hospitali.




Kwa wale waliopitia Jeshi, ona picha hii (Katikati) Meja Haniu akiwa na maafisa wenzake toka Kambi ya JKT Mlale, Songea Vijijini. Kambi hiyo ni maarufu sana kwa uzalishaji wa mahindi na mwaka huu wameanza kuzalisha Mbegu za mahindi. Mashamba kule yana majina kama Embakassy nk. Kutokana na kazi nzuri Kambi hiyo ilipendekezwa wapewe trekta kusaidia kuzalisha mbegu bora za mahindi.



Saturday, October 9, 2010

Mkono wa Kwaheri--Rais KIKWETE na Dkt Nchimbi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akiagana na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (katikati Mwenye kofia kijani) Mwenyekiti wa Chipukizi Mkoa wa Ruvuma, Alina Mfaranyaki ambaye alisalimiana pia na rais kwa kutambulishwa na Dkt Nchimbi. (Picha na Muhidin Amri--Ndolanga)
Rais wa CWT Taifa, Comred Gratian Mukoba (Katikati) akiweka saini Kitabu cha wageni cha Ruvuma Press Club, (Kulia) ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Juma Nyumayo ambaye alipokea shukurani za rais huyo kwa kazi nzuri iliyofanywa na wanahabari wa mkoa wa Ruvuma katika kufanikisha na kuhabarisha umma kuhusu maadhimisho ya siku ya Mwalimu Duniani kitaifa mkoani Ruvuma Oktoba 5, 2010 (Picha na Muhidin Amri- Ndolanga)

Usijemuahidi mwenye upere kucha. DC atolewa mkuku Maghala ya Hifadhi ya chakula Ruhuwiko

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Savery Maketa, (Mwenye Suti) akizomewa na wakulima wanaosotea kuuza mahindi yao kwa wiki tatu sasa katika Maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula Kanda ya Songea Ruhuwiko Manispaa ya Songea jana (Picha na Muhidin Amri-Ndolanga) Tatizo la soko la mahindi mkoani hapa limechukua sura mpya ambapo watu wanakesha usiku na mchana kusotea kuuza mahindi yao, Dc huyo alionekana kama bughudha na hana uwezo wa kuwasaidia hivyo kutimuliwa kama muionavyo hiyo picha. Dada Yasinta na mnaofuatilia Blog yenu hii mmeona mambo hayo?

Mapokezi ya Kikwete CWT Songea na Mahafali ya Shule Luhira

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi wasioona na wanaoona luhira manispaa ya Songea akitoka katika Choo iliyojengwa kwa msaada wa Shule ya Trinity-Scotland chini ya usimamizui wa Rev. Martin Mlata was GSM Songea. Mgeni Rasmi katika mahafali ya darasa la Saba Shule ya Msingi Luhira manispaa ya Songea, Rev Martin Mlata, akimpatia cheti mmoja wa wanafunzi Jafua juma Nyumayo jana ambapo Mchungaji huyo aliwaomba wazazi wasiwafiche watoto wenye ulemavu na watumie kamati za shule kutatua matatizo yanayowakabili katika kuendeleza elimu.
Mhe. Rais Jakaya kikwete, anayefungua pazia kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la walimu (CWT) Mkoawa Ruvuma huku Rais wa CWT Mwalimu Gratian Mkoba katikati na Prof Jumanne Magembe, Waziri wa Elimu na Mafunzio ya Ufundi wakimwangalia. Jengo hilo lipo Mkabala na Jengo la Saccos ya walimu Mtaa wa Zanzibar Manispaa ya Songea.


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma, Juma Nyumayo (Kushoto)akisalimiana na Kamanda wa Brigedi ya Kusini (Tembo) Brigedia Igoti, ambaye amerejea toka Masomoni nchini China hivi karibuni.



Maafisa wa Mawasiliano toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi toka Kushoto, Juma Nyumayo, toka Kituo cha Songea, Magdalena Kishiwa toka Dar es Salaam na wa Mwisho Christian Sikapundwa Mhariri wa magazeti vijijini Kanda ya Kusini wakiwa Uwanja wa Ndege kumpokea Rais Kikwete Oktaba 5, 2010.


Baadhi ya Wafanyakazi waJengo la SACCOS ya walimu Songea Vijijini wakiwa pamoja na Beatrice Sweetbert wa Kagimbo Enterprises Mjini Songea (wa kwanza Kulia aliyeshika kiuno akiwa na shangazi yake mama Julie aliyeshika mfuko wa rambo) wakimsubiri Rais Kikwete katika eneo la tukio la kuzindua na kufungua rasmi Jengo la walimu CWT Mkoa wa Ruvuma Oktoba 5, 2010









Sunday, October 3, 2010

VITU TOFAUTI VIONJO TOFAUTI

Picha ya kwanza ni ya Boss wa TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Bw. Christian Sikapundwa mara baada ya kufungua Blog ya TUJIFUNZE KUSINI. Huu ni uharibifu mkubwa wa mazingira, moto huo ulikuwa unawaka katika misitu ya Lilondo tarafa ya Madaba Songea Vijijini jana wakati tunarudi toka Dar na Bus la Super Feo hakika wanakijiji walipagawa kuuzima lakini wapi maana kila pembe na ujuavyo miti ya kupanda inavyopwaka utafikiri petroli Boss wangu kaniambia aliyechoma anajisifu eti ana mkono mkali.


Jamani uzuri ulioje sifa apewe Bwana kwa uumbaji hapa ni Shamba la Chai Kibena pale Njombe , unajua dereva akasema teremkeni mkachimbe dawa mie nikauona uzuri huo na huyo Bwana ni Mlonda au mlinzi wa shmba hilo lakini yeye halijui jina lake.

Picha ya Kushoto ni Bw. Adam Nindi katikati ni Bw Kiim ambaye ni Msanii wa uchoraji lakini pia ana asilia ya mkoa wa Ruvum,a na huyo kulia ni Juma Nyumayo Mwenyekiti wa ruvuma Press Club wakishauriana jambo kuhusu harakati za kijinsia katiak darasa Mojawapo la TGNP Dar es Salaam. picha hiyo ilinitetemesha sana hata kupiga sikuamini kuwa hapo ni Dar ni nyuma tu ya kiwanda cha Urafiki Dar es Salaam. Bongo nayo ipio hivyo je madongo poromoka ya mikoani inakuwaje.
(Picha zote na Juma Nyumayo)









Dr Slaa na Mkewe Josephine walivyotesa Ruvuma


Penye mafanikio ya Mwanamume mwanamke yupo! hapa Josephine Mshumbusi mke wa Dr Willbrod Slaa akisalimia wananchi na kumuombea Kura mmewe dr Slaa katika viwanja vya Majengo manispaa ya Songea. Mkutano huo ulifunikwa na watu kibao dalili zilizojitokeza wazi kukunwa na mgombea huyo ambaye ni tishio hasa mijini (Picha na Christian Sikapundwa)

Mwenge Ulivyopita Ruvuma 2010


Huyo Mwenye furaha na kumshika mkono mkimbiza Mwenge kitaifa ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Ruvuma Bw. Cornelius Msuha kushotowake ni Dr. Tarimo ambaye ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma

Friday, October 1, 2010

KIONGOZI WA TGNP USU MALYA


Huyu ndio Boss wa TGNP mtumishi wa watu mwenye Mtazamo wa kijinsia Dada USU MALYA akiwaasa waandishi wa habari na wasanii waliohudhuria Mafunzo ya kutathimini kazi walizojipangia Mwezi March mwaka huu na matokeo yake waendelee kujituma katika Vuguvugu la kimapinduzi la kumkomboa mwanamke wa Pembezoni. Mafunzo hayo yalifanyika TGNP Mabibo DSM
(Picha na Juma Nyumayo)

Hii ni foleni toka Ubungo mataa hadi Kona kuelekea Kimara


Jamani Dar napo hapafai. Nilikuwa niwahi kule TGNP eneo la Mabibo. Nilipofika barabarani nikakuta hali hiyo. Nikaamua kuchukua Pikpiki kule Songea tunaita yeboyebo na maeneo mengine Bodaboda. Yasinta unayefuatilia mtandao huu na wenzako Mpo hapo? sijui nyie huko majuu mambo yapoje? kuna haja ya kuweka mipango na mikakati ya kuendeleza miundombinu ya barabara pia kujenga setlite towns. (Picha na Juma Nyumayo)

Jaji Mkuu wa Tanzania na wadau wa Habari Blue pearl DSM

Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhani (Mwenye suti nyeusi waliokaa katikati) akimwangalia Mzee lifa Chipaka hasimu mkubwa wa Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere na ndiye Kiongozi wa Chama Cha TADEA walipopiga picha ya pamoja na wadau wahabari katika Mkutano ulioandaliwa na Misa-Tan na UNDP kuweka sawa uwanja wa habari katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huu. (picha na Juma Nyumayo)

Mambo ya TGNP katika kuwasilisha

Waandishi wa Habari wakiwakilisha kazi zao leo hapo TGNP wa kwanza kulia ni Sima bengileki toka Iringa Press Club, katikati aliyesimama ni Spear Patrick wa majira na aliyekaa ni Lilian Liundi wa TGNP akifuatilia na kuchukua point za visa mkasa vilivyowakilishwa na waandishi hao kufuatia mpango kazi waliouweka March mwaka huu kuhusu Vuguvugu la Kimapinduzi kumkomboa mwanamke wa pembezoni atumie rasilimali.
(Picha na Juma Nyumayo)

Wednesday, September 29, 2010

Mahafali kidato cha nne Sekondari ya Msamala

Mama anapomzawadia bint yake akiwa amehitimu zsafari ya miaka 4. pichani Amina Nyumayo aliyekuwa anasoma sekondari ya Msamala manispaa ya Songea akipokea zawadi toka kwa mama yake Mzazi wakati wa mahafali ya sita ya Shule hiyo wiki iliyopita. (Picha na Maelezo na juma Nyumayo)

Monday, September 20, 2010

Unapajua hapo?




Wakati wa kampeni raha kama nini, je baada ya uchaguzi watapita humo. Hapa ni Mto Ruhuhu Mkoani Ruvuma na JK akishuka katika ardhi ya Mbeya Vijijini (Picha zote kwa hisani ya http://www.kalulunga.blogspot.com/)

Mambo ya Gemsat Kurasini!

Heheheee! Nimekutana na waandishi kibao toka Zanzibar tulikuwa Ali Othman na Haroub Hussein kule Tanga tulikuwa na Anna Makange pamoja na wengine wengine.

Saturday, September 18, 2010

Dorothy Mbilinyi wa TGNP ndani ya RUVUMA

Mama Dorothy Mbilinyi, (aliyekaa katikati) kaanza kazi mara moja kwa kueleza nini anatarajia kufanya katika mafunzo ya jinsia na Demokrasia hapa Ruvuma, katika picha anaonekana akihesabu point za kusisitiza kwa viongozi wa Dini mbalimbali na Mashirika yasiyo ya kiserikali. Wengine waliosimama Ni Steve Chindiye wa Ruvuma Press, Juma Nyumayo wa RUNECISO Fatuma Lazaro wa UDSM na Elizabeth Mbena wa UDSM aliyekaa kulia kabisa ni Judith Lugoye.
Mpiga Picha wa Gazeti la Mtanzania Bw Muhidin Sufiana (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Juma Nyumayo baada ya kutembelea ofisi za Chama cha Waandishi wa habari mkoani hapa, hivi karibuni. wenginme ni happy Katabazi wa Tanzania daima na Editha Karlo wa Mtanzania.


Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF Mgombea Urais Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, 2010 akitoa sera kwa wananchi katika ngome ya CHADEMA viwanja vya stendi ya malori Majengo Manispaa ya Songea.
Picha nyingine baadhi ya watoto na watu wazima waliofika katika viwanja hivyo kusikiliza sera za CUF. (Picha zote na Muhidin Amri- Ndolanga)






Friday, September 17, 2010

JIONEE MWENYEWE MAMBO YALIVYO

Mama Lishe wa Manispaa ya Songea ambaye jina lake halikuweza kufahamika mala moja akimlisha chakula Mtoto wake.

Muuza samaki wa bichi kutoka Ziwa Nyasa akitembeza Samaki hao kwa nia ya kuboresha Lishe za wateja wake.


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Eliza Mbena na Fatuma Lazaro wakivishana Vitambaa vya Chama Tawala CCM
Kijana akipata Chakula kutoka kwa mama Lishe katika eneo la Standi ya Mabasi katika Manispaa ya Songea