Wednesday, July 10, 2013

NANI KAMA LOWASSA? ACHANGISHA FEDHA AVUKA MALENGO MWANZA

PATA PICHA NA MAELEZO KAMILI


GUMZO LENYEWE
Picha hizo za Lowassa ambazo zimeenea mtandaoni, zimepokea maoni mbalimbali huku wengi wakiwa na maswali yaliyokosa majibu ya moja kwa moja.
Hata hivyo, asili ya picha hizo zilizombadilisha mwonekano Lowassa ni mtandao mmoja wa kijamii ambao umetupia picha na maelezo kwamba, mbunge huyo ambaye kasi yake ya kisiasa nchini haishikiki, alikuwa akipongezwa na Kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho na kilemba baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza. 

ENEO LA TUKIO
Ishu hiyo ilijiri usiku wa Ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza hivyo kuondoa utata kwamba, alivaa vazi hilo na kuzama nalo msikitini kitendo ambacho baadhi ya watu walisema si sahihi kama mheshimiwa huyo hajabadili imani yake. Lowassa ni wa imani ya KKKT.NA GLOBAL PUBLISHER

ACHANGISHA FEDHA, AVUKA MALENGO
Katika harambee hiyo, Lowassa aliyekuwa jijini humo sanjari na wafanyabiashara wengine wa karibu yake, alifan
ikisha wadau kuchangia shilingi milioni 590 hivyo kuvuka lengo la milioni 500. Kwa hiyo shilingi milioni tisini zilizidi.
Kufuatia hali hiyo, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na baadhi ya viongozi wa Kiislam ili kuwasikia wanaliongeleaje tuko la Lowassa kuvaa vazi hilo.

SKU zilizopita kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, picha za Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa akiwa amevaa mavazi ya Kiislam ya joho na hagali zimezua gumzo kubwa kwenye jamii wengi wakitaka kujua kama Waziri Mkuu Mstaafu huyo amebadili imani au la !.

Akizngumza na gazeti hili juzi, Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Simba alisema kitendo anachofanya Lowassa cha kusaidia jamii ni cha kiungwana na kinakubalika kwa kuwa analisaidia taifa.

“Kusaidia jamii kunakubalika na kila mtu na tunataka watu kama Lowassa wawe wengi katika nchi yetu. Narudia tena kusaidia jamii si vibaya hata kidogo tuige mfano huo,” alisisitiza Mufti Simba.

SHEHE WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa akizungumzia tukio hilo alisema ni jema  kwa kuwa alichochangia Lowassa kitasaidia jamii ya Watanzania.

“Mheshimiwa Lowassa amechangia redio na kama itatumika vizuri taifa zima la Tanzania litafaidika. Amefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuliiga. Ieleweke hakuchangia ibada kachangia huduma za jamii,” alisema shehe huyo.

SHEHE WA MKOA WA MWANZA
Naye Shehe wa Mkoa wa Mwanza ambako tukio la Lowassa lilifanyika, Salum Hassan Fareji kwa upande wake alimpongeza kiongozi huyo kwa uamuzi wake wa kuchangia redio hiyo kwa kufanya harambee iliyozaa matunda. “Alichokifanya (Lowassa) ni faraja kubwa kwetu sisi kama viongozi wa Kiislam, tunamuomba aendelee kuhudumia jamii,” alisema.

KIONGOZI WA SUNNI
Kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein Al Badawi amesema kitendo alichokifanya Lowassa ni thawabu kubwa kwa Mwenyezi Mungu na amewataka watu wengine kuiga uungwana huo.

JAMII INASEMAJE?
Baadhi ya Watanzania waliozungumza na Risasi Mchanganyiko kwa nyakati tofauti walisema kwao kiongozi kuchangia jamii ni vyema tu, mbaya kama katika kuchangia huko atakuwa anapiga kampeni ya nafasi au cheo anachokifukuzia.

“Mimi sidhani kama kuna tatizo, kiongozi yeyote anatakiwa kuisaidia jamii, awe tajiri au wa kipato cha kawaida, tatizo litaibuka kama kiongozi huyo atatumia nafasi hiyo kufanya kampeni,” alisema Slim Abood, mkazi wa Kijitonyama Dar.
    
KUHUSU LOWASSA
Siku za hivi karibuni, Mheshimiwa Lowassa amekuwa akifanya harambee mbalimbali kuchangia jamii. Maeneo ambayo amekuwa akiyagusa zaidi ni nyumba za ibada na makundi ya akina mama, lakini hivi karibuni alikutana na Machinga wa Jiji la Mwanza ambao aliwaahidi kuwajaza ‘mafedha’ kwa ajili ya kujiinulia vipato vyao.

NI KUUSAKA URAIS ?.
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya watu wakivitumia vyombo vya habari wamekuwa ‘wakitabiri’ kwamba, Lowassa anafanya harambee hizo kwa lengo la kuusaka urais wa Tanzania mwaka 2015.

Hata hivyo, Lowassa mwenyewe hajawahi kuweka wazi msimamo wa kugombea urais mwaka huo. 

LOWASSA AZUNGUMZA NA RISASI MCHANGANYIKO
Baada ya yote, Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya kuzungumza na Mheshimiwa Lowassa kwa njia ya simu ya kiganjani na kumuuliza nini madhumuni yake ya kufanya harambee ya kuchangia redio hiyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nimeamua kufanya harambee ile kwa sababu ni redio ya dini. Unajua unapochangia redio ya dini, yoyote ile maana yake itaweza kutoa vipindi bora vya kuelemisha jamii yote.
via/jumamtanda blog

No comments:

Post a Comment