Thursday, July 4, 2013

JESHI LA MISRI LAMWANGUSHA RAIS MURSI KWA KUKAIDI USHAURI ALIOPEWA


 HATMA YA AFRIKA: MAPINDUZI NA UJENZI WA DEMOKRASIA  KATIKA MATAIFA YA KIARABU. Egypt's Chief of Staff General Abdulfettah es Sisi announced the president of the constitutional court to task presidency until the elections. (video captured) (Anadolu Agency - Egyptian TV) 
Keine Weitergabe an Drittverwerter.
MAELFU ya Wamisri wanasherehekea kupinduliwa Rais Mohammed Mursi, huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi limeanza kuwakamata viongozi wa juu wa Udugu wa Kiislamu na wasiwasi ikiwa hatua hii italeta muafaka wa kisiasa. 

Kwa siku nzima ya jana (03 Julai), watu walikuwa wakisubiri kwa hamu muda wa mwisho aliopewa Rais Mursi na jeshi, na jioni yake maelfu ya wapinzani wa kiongozi huyo wa mwanzo kuchaguliwa kidemokrasia walizidi kumiminika kwenye viwanja vya Tahrir na kasri ya rais. 

Hali ilikuwa ya amani zaidi kuliko ilivyokuwa katika siku za hivi karibuni.

Pale waziri wa ulinzi alipoanza kutoa hotuba yake iliyongojewa kwa hamu na kwa muda mrefu, umma ulip
iga kelele za “Amani!Amani!”, lakini dakika chache baadaye umma huo ukaripuka kwa vifijo na nderemo na uwanja wa Tahriri ukageuka mara moja kuwa uwanja wa tamasha. 

Fashifashi zikalitanda anga, na watu wakavaana miilini huku wakifuta machozi ya furaha. Sharif, profesa wa chuo kikuu ni mmoja wao.

“Nina furaha ya kunichania nguo hapa, kuona kwamba Wamisri wa kila tabaka wapo uwanjani. 

Mtu anaweza kusema kwamba huku ni kuachiliwa uhuru wetu kutoka gerezani mwa wenye siasa kali. Udugu wa Kiislamu wamesababisha matatizo mengi sana.” Amesema Sharif.

Sharif alisisitiza kwamba wote ni Wamisri na sio Waislamu au Wakristo, kwamba kwa miaka 7000 wamekuwa wakinywa maji mamoja na wakivuta hewa moja. Kando ya Sharif, mtu mwengine alijiangusha chini na kusujudu kumshukuru Mungu, huku macho yake yamerowa machozi.

Bado kungali na maswali kadhaa
Maafisa wa jeshi wakishangiria baada ya Mursi kutangazwa amepinduliwa. Maafisa wa jeshi wakishangiria baada ya Mursi kutangazwa amepinduliwa.
 
Lakini kando ya furaha hizi kubwa, watu hawa waliopeperusha bendera kulipongeza jeshi kwa kumuondoa Mursi, bado wana maswali kadhaa ya kujijibu. Jeshi, upinzani, wawakilishi wa Kanisa la Koptik na wa dini ya Kiislamu, walisema wamekubaliana kwamba Mkuu wa Mahakama ya Kikatiba awe rais wa kipindi cha mpito, lakini utaratibu mzima kuelekea uchaguzi mpya bado hauko wazi.

Pia haifahamiki hatima ya Rais Mursi na wenzake wa kundi la Udugu wa Kiislamu, ambao taarifa zinasema wanashikiliwa na jeshi. Baadhi ya walio Uwanja wa Tahriri, kama Nadir, wanapajua wanapotaka Mursi awepo kwa sasa.

“Lazima awe yuko gerezani na lazima mumshitaki. Watu wengi wameuawa wakati wa uongozi wake na hatuwezi kuwasahau.” Anasema Nadir.

Lakini Mursi alikuwa rais wa kwanza kuingia madarakani kupitia uchaguzi wa kidemokrasia, akishinda zaidi ya asilimia 50 ya kura, na hivyo uhalali na nguvu zake haziwezi kupuuziwa kisiasa na hata kisheria.

Bado haifahamiki ikiwa wafuasi wa Udugu wa Kiislamu, ambao waliripuka kwa ghadhabu wakati mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, alipokuwa akitangaza mapinduzi yake usiku wa jana, watajiunga na kipindi cha mpito, ama nao wataendelea kuandamana na hivyo kuikwamisha tena nchi kisiasa.

Kwa vyovyote vile, bado mambo hayajesha kwenye taifa hilo kongwe kaskazini mwa Afrika.
via/jumamtanda blog

No comments:

Post a Comment