Jamaa wataka
kafara mtu, wapate maji
Na Steven
Augustino, Tunduru
KATA ya
Namasakata Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imesema kuwa ipo tayari kutoa kafara
damu ya mtu ili kupata maji.
“tupo tayari mtu
achinjwe kwa ajili ya tambiko litakalo
sadia Wananchi wa kata yetu kupata huduma ya maji safi na salama,”.
Kauli jiyo ilitolewa
na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Masache Ally, aliye
mwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilayaya Tunduru Mhe. Faridu Khamisi, ambaye alimweleza Mkuu wa
Wilaya hiyo, Bw. Chande Nalicho, kwamba
kauli hiyo ameitoa kufuati Serikali kuwapiga danadana kila wanapo ahidi kuwapelekea
huduma za maji safi na salama.
“…sisi wananchi
wa kata Namasakata tumejiandaa na tuko tayari kumtoa hata mtu mmoja miongoni
mwetu ili auawe kwa kuchinjwa na damu yake imwagike na kutumika kama kafara
itakayo fanikisha kupatikana kwa maji na kuwaondolea kero wananch wa vijiji vya
Namasakata na Mkasale” alisema Mhe. Diwani Masache.
Akifafanua kauli hiyo Mhe. Masache alisema kuwa mbali na
vijiji hivyo kushirikiana na wataalamu katika utafiti lakini wameishia kuahidiwa
kupelekewa miradi ya maji ambayo haijatekelezeka kwa muda mrefu hali inayo
wafanya wananchi kukata tamaa na kuhisi labda kuna mkono wa mtu.
Wakizungumzia
hali hiyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Namsakata Bw.Yusuf Mkali, na Mkazi wa Kijiji
cha Mkasale aliyejitambulisha kwa jina la Nuru Hasani waliosema kuwa Vijiji
hivyo vinakabiliwa na hali mbaya ya upatikanaji wa maji tangu mwaka 1982 kiasi
cha kutishia maisha ya wakazi wake.
Walisema, upande wa Kijiji cha Mkasale hali ni mbaya
zaidi kutokana na kuwepo kwa shubiri ambayo huwapata akina mama wanaokwenda
kujifungua katika Kituo cha Afya ambapo hulazimika kwenda kuchota maji Mtoni
umbali wa zaidi ya Kilometa 2 huku wakiwa katika hatari ya kujeruhiwa ama
kuuawa na wanyama wakali ambao pia huyatumia maji hayo kunywa.
Akiongea katika
maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya
Tunduru, Bw. Chande Nalicho, alimtaka
Mhandisi wa Idara ya maji Wilayani humo, Eng. Paschal Kidiku, kushirikiana na wataalamu kufanya utafiti na
kutoa majibu ya uhakika kwa wananchi hao ili wajue na kutoa maamuzi ya kukihama
kijiji chao ama la.
Awali akisoma
risala ya maadhimisho hayo kwa niaba ya Mhandisi wa maji wilaya ya Tunduru, Eng. Paschal Kidiku, Bw. Kasim Dinny, aliye mwakilisha Mhandisi huyo alikili kuwa
Vijiji hivyo vinakabiliwa na tatizo hilo kwa kiasi kikubwa na kwamba na kwamba
hali hiyo inatokana na maji kupatikana mbali wa kina kirefu hali ambayo
inawafanya wataalamu kuumiza vichwa jinsi gani wataweze kulitatua tatizo hilo
baada ya miradi ya uchimbaji wa visima 7 kutoa maji kidogo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment