Sunday, March 24, 2013

Mvua Dar zasumbua, vijana wajipatia kipato


 Mvua zilizonyesha Jumapili Machi 24, zilisababisha maafa kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam.  
Maafa hayo ni pamoja na watu kupoteza mali zao, baadhi ya miundombinu kuharibika mfano daraja  la mto Kilungule ambalo lilifunikwa na kuzibwa na takataka kiasi cha watu kushindwa kupita kwa baiskeli, bodaboda na magari na kusababisha usumbufu mkubwa. Hali iliwafanya vijana wa eneo hilo kuchamkia kusafisha daraja hilo punde maji yalipopungua na kuweka vizuizi na kutoza kiasi cha Shilingi 500 kwa kila chombo cha usafiri. Fedha hiyo iliwekwa hadharani kuonyesha uhalali wa kazi yao jambo lililopelekea Mwenyekiti wa serikali ya mtaa aliyefahamika kwa jina moja la Baba Hamisi kuingilia kati na kutaka waache kutoza fedha kwa wavukaji jambo ambalo vijana hao walilipinga vikali na kuendelea kuweka vizuizi na kutoza fedha. Eneo la Manzese Tiptop wafanya bishara wengi wamekula hasara baada ya maji kuingia kwenye maduka na kuharibu bidhaa mbalimbali.
 (Stori na picha kwa hisani ya Christopher Juma)


No comments:

Post a Comment