Monday, March 25, 2013

Kamishna wa Tume Mabadiliko ya Katiba azitaka asasi kusoma rasimu ya Katiba mpya

Maelezo ya Picha ya Kwanza ni Mwenyekiti wa Maboresho na Utetezi Bw. Harold Sungusia, Picha ya Pili ni Kamishna wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Bw. Humphrey Polepole, (Mwenye saa Mkononi) Picha ya tatu ni baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye Chumba cha Mkutano hivi karibuni Jijini Dar.



Na Juma Nyumayo, Dar. Kamishna wa Tume ya mabadiliko ya Katiba nchini, Bw. Humphrey Polepole(Pichani juu), amewaomba viongozi wa Azaki nchini kuendelea kutoa elimu kwa wananchi umuhimu wa kusoma Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, na kuisoma Rasimu ya Katiba mpya na kutoa maoni  kupitia Mabaraza ya Katiba yatakayoundwa. Bw. Polepole aliyasema hayo wakati akitoa mada ya Muundo wa Mabaraza ya Katiba katika Ukumbi wa Kituo cha Haki za Binadamu -LHRC- Kijitonyama Dar Es Salaam.
Awali akifungua Mkutano huop amabao uliwashirikisha viongozi toka Mitandao ya mashirika yasiyo ya kisewrtikali ya Mikoa, Mashirika ya Kitaifa na ya Kisekta hapa nchini chini ya Uratibu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini NACONGO kwa Ushirikiano na Kituo hicho cha LHRC, Mwenyekiti wa Maboresho na Utetezi, Bw. Harold Sungusia. alisema kila mtu anawajibu wa katika kutengeneza katiba mpya na kuleta mabadiliko.


Nikiwa na G Sengo wa Clouds Mwanza

Bw. G Sengo, Mwanahabari machachari mwenye vipaji Kibao. Sengo ni Bloger pia ni MC wa Nguvu katika Shughuli mbalimbali zenye Mvuto Jijini Mwanza. jambo linalovutia zaidi Sengo ni Mtangazaji na ni Mwanhabari wa Clouds FM Mwanza. (Pichani kushoto akishangaa jambo baaada ya mimi Juma Nyumayo- Kulia kumtonya wakati picha ikipigwa kwenye hafla ambayo ilikuwa akiindesha yeye kama Msema Chochote, (MC) aliyefanikisha sana shughuli hiyo iliyohudhuriwa na watu mashuhuri wakiongozwa pia na  Wakuu wa madhehebu mbalimbali. (Picha na  Bw. Hassan Hashim wa Tanga Press Club.)

Sunday, March 24, 2013

Mvua Dar zasumbua, vijana wajipatia kipato


 Mvua zilizonyesha Jumapili Machi 24, zilisababisha maafa kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam.  
Maafa hayo ni pamoja na watu kupoteza mali zao, baadhi ya miundombinu kuharibika mfano daraja  la mto Kilungule ambalo lilifunikwa na kuzibwa na takataka kiasi cha watu kushindwa kupita kwa baiskeli, bodaboda na magari na kusababisha usumbufu mkubwa. Hali iliwafanya vijana wa eneo hilo kuchamkia kusafisha daraja hilo punde maji yalipopungua na kuweka vizuizi na kutoza kiasi cha Shilingi 500 kwa kila chombo cha usafiri. Fedha hiyo iliwekwa hadharani kuonyesha uhalali wa kazi yao jambo lililopelekea Mwenyekiti wa serikali ya mtaa aliyefahamika kwa jina moja la Baba Hamisi kuingilia kati na kutaka waache kutoza fedha kwa wavukaji jambo ambalo vijana hao walilipinga vikali na kuendelea kuweka vizuizi na kutoza fedha. Eneo la Manzese Tiptop wafanya bishara wengi wamekula hasara baada ya maji kuingia kwenye maduka na kuharibu bidhaa mbalimbali.
 (Stori na picha kwa hisani ya Christopher Juma)


Saturday, March 23, 2013

Wataka kutoa kafara mtu kisa maji



Jamaa wataka kafara mtu, wapate maji
Na Steven Augustino, Tunduru
KATA ya Namasakata Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imesema kuwa ipo tayari kutoa kafara damu ya mtu ili kupata maji.
“tupo tayari mtu  achinjwe kwa ajili ya tambiko litakalo sadia Wananchi wa kata yetu kupata huduma ya maji safi na salama,”.
Kauli jiyo ilitolewa na Diwani wa Kata hiyo Mhe.  Masache Ally,  aliye  mwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilayaya Tunduru  Mhe. Faridu Khamisi, ambaye alimweleza Mkuu wa Wilaya hiyo,  Bw. Chande Nalicho, kwamba kauli hiyo ameitoa kufuati Serikali kuwapiga danadana kila wanapo ahidi kuwapelekea huduma za maji safi na salama.
“…sisi wananchi wa kata Namasakata tumejiandaa na tuko tayari kumtoa hata mtu mmoja miongoni mwetu ili auawe kwa kuchinjwa na damu yake imwagike na kutumika kama kafara itakayo fanikisha kupatikana kwa maji na kuwaondolea kero wananch wa vijiji vya Namasakata na Mkasale” alisema Mhe. Diwani Masache.
Akifafanua  kauli hiyo Mhe. Masache alisema kuwa mbali na vijiji hivyo kushirikiana na wataalamu katika utafiti lakini wameishia kuahidiwa kupelekewa miradi ya maji ambayo haijatekelezeka kwa muda mrefu hali inayo wafanya wananchi kukata tamaa na kuhisi labda kuna mkono wa mtu.
Wakizungumzia hali hiyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Namsakata Bw.Yusuf Mkali, na Mkazi wa Kijiji cha Mkasale aliyejitambulisha kwa jina la Nuru Hasani waliosema kuwa Vijiji hivyo vinakabiliwa na hali mbaya ya upatikanaji wa maji tangu mwaka 1982 kiasi cha kutishia maisha ya wakazi wake.  
Walisema,  upande wa Kijiji cha Mkasale hali ni mbaya zaidi kutokana na kuwepo kwa shubiri ambayo huwapata akina mama wanaokwenda kujifungua katika Kituo cha Afya ambapo hulazimika kwenda kuchota maji Mtoni umbali wa zaidi ya Kilometa 2 huku wakiwa katika hatari ya kujeruhiwa ama kuuawa na wanyama wakali ambao pia huyatumia maji hayo kunywa.
Akiongea katika maadhimisho hayo,  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,  Bw. Chande Nalicho, alimtaka Mhandisi wa Idara ya maji Wilayani humo, Eng. Paschal Kidiku,  kushirikiana na wataalamu kufanya utafiti na kutoa majibu ya uhakika kwa wananchi hao ili wajue na kutoa maamuzi ya kukihama kijiji chao ama la.
Awali akisoma risala ya maadhimisho hayo kwa niaba ya Mhandisi wa maji wilaya ya Tunduru,  Eng. Paschal Kidiku,  Bw. Kasim Dinny,  aliye mwakilisha Mhandisi huyo alikili kuwa Vijiji hivyo vinakabiliwa na tatizo hilo kwa kiasi kikubwa na kwamba na kwamba hali hiyo inatokana na maji kupatikana mbali wa kina kirefu hali ambayo inawafanya wataalamu kuumiza vichwa jinsi gani wataweze kulitatua tatizo hilo baada ya miradi ya uchimbaji wa visima 7 kutoa maji kidogo.
Mwisho

Wednesday, March 6, 2013

Mkuu wa Mkoa anapokutana na Mhariri Tujifunze

Kusalimiana na furaha juu 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akisalimiana na mhariri wa gazeti la Tujifunze Kanda ya Kusini, Bw. Christian Sikapundwa, hivi karibuni mjini Songea


Nilipokuwa viwanja vya Mashujaa wa vita vya Majimaji

Mara nyingine  tene, Juma Nyumayo (Pichani)  nilikuwepo kwenye viwanja vya Mashujaa wa Vita vya Majimaji Manispaa ya Songea kuhudhuria Tamasha la Kumbukizi la Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni. Kwaujumla mambo yalikuwa mazuri sana. Zuria jekundu kwaajili ya Mgeni Rasmi, Mhe. Balozi hamis Kagasheki, Waziri wa maliasili na Utalii. Watu wenyewe pia walivalia nguo nyekundu na vitambaa vyekundu ishara ya wapiganaji wakingoni.