Monday, March 29, 2010

Katibu Mtendaji TACOSODE anaposisitiza jambo!

Katibu Mtendaji wa Tanzania Council for Social Development (Tacosode) amesema ni muhimu kwa wananchi na serikali zao kushirikiana kwa karibu katika kufuatilia Rasilimali za Umma kwa maendeleo.
hayo ameyasema katika Ukumbi wa VETA Mjini Songea wakati akifungua mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii wa kufuatilia matumizi ya fedha za umma katika Manispaa ya Songea, Wilaya za Namtumbo, Songea vijijini , Mbinga na Tunduru.
Bibi Kapinga amesema ni jukumu la watu kuhakikisha wanafuatilia mipango na utekelezaji wa shughuli zote kwa njia shirikishi kwani maendeleo ya kiuchumi na kijamii hayatafikiwa iwapo wananchi hawatajua namna ya rasilimali zao zinavyotumika na ushiriki ulivyo.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na mada mbalimbali wanazojifunza wamevutiwa sana uamuzi wa Baraza la vyama vya Hiari na Maendeleo ya Jamii TACOSODE kwa uamuzi wa kuendesha mafunzo hayo mkoani Ruvuma kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society.
Akielezea umuhimu wa uamuzi huo kwaniaba ya wakazi wa Ruvuma, Katibu wa Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali wilaya ya Songea SONNGo Bw. Mathew Ngalimanayo alisema Tacosode imechukua uamuzi ambao AZIse nyingi hazijawahi kuthubutu "Tacosode wameanza kuonyesha njia, tunaomba pia mashirika mengine yafuate nyayo ili kuharakisha maendeleo mikoa ya pembezoni," alisema na kumpongezaKatibu Mtendaji Theofrida Kapinga kwa kutoa wito kwa wanaRuvuma kujenga mahoteli mazuri kwaajili ya wageni.
Alifikia hatua hiyo kwakuwa wageni ndio huleta chachu ya maendeleo katika maeneo husika.

No comments:

Post a Comment