Wednesday, December 18, 2013

LAKE OIL LTD KUFUNGUA MAUZO YA MAFUTA SONGEA

Mtumishi wa lake Oil Ltd, Bw. Moses Clemency, akiwa mbele ya moja ya Pampu mpya za mafuta katika Kituo hicho kilichopo eneo la Manzese, Manispaa ya Songea.

KAMPUNI ya mafuta Lake Oil Ltd ya Dar es Salaam, imefungua Kituo cha mafuta Manispaa ya Songea.

Kituo hicho kilichopo Mkabala na Ofisi za Zimamoto na kuangaliana na Soko la Wakulima Manzese mjini hapa, kimebadili Sura ya eneo hilo kutokana na Ukarabati na kujenga paa kubwa katika Pampu mpya za mafuta aina ya Diesel, Petroli na ya taa.

Kwa Mujibu wa Meneja wa Kituo hicho, Bw. Daud Mmasa Sevuri, alisema kuwa huenda Alhamisi wiki hii wakaanza kuuza mafuta kwa bei nafuu wakilinganisha na vituo vingine mjini hapa.
"Alhamisi wiki hii tunatarajia kuanza kuuza mafuta hapa songea," alisema.

Ujio wa Kampuni ya Lake Oil Mkoani hapa, utaongeza ushindani wa Biashara ya mafuta ya mitambo na Gas kwa matumizi mbalimbali na kusaidia kusukuma maendeleo ya sekta ya kilimo, madini, usafiri na utoaji huduma.

Mkoa wa Ruvuma haujaunganishwa na Umeme Grid ya taifa hivyo kuufanya kutegemea zaidi mafuta.
Kilio kikubwa cha wakazi wa mkoa huu kitabaki kupata wakala wa kuuza mafuta ya ndege.
Angelipatikana wakala huyo Uwanja wa ndege ulioko eneo la Ruhuwiko manispaa ya Songea, wenye ubora wa kutua ndege mbalimbali isipokuwa Boeng,  ungeweza kutumika ipasavyo kwa abiria na kupunguza gharama ya nauli wanayolipa sasa kwa kutumia ndege ndogo.

No comments:

Post a Comment