Friday, May 28, 2010

Pilika za Mapokezi ya Balozi wa Sweden Ruvuma!












Hizi ndio Shangwe na pilikapilika za ujio wa balozi wa Sweden nchini, Mheshimiwa Staffan Herrstom aliyezulu mkoani Ruvuma.
maandalizi hayo yalifanywa kwa ushirikiano kati ya Ruvuma Press Club na Makumbusho ya Taifa ya Majimaji.
Picha ya kwanza Mkurugenzi wa Makumbusho hayo Bw. Philip Maligissu akimkaribisha balozi Herrstom huku Mlezi wa Ruvuma Press Club Mbunge Eng. Stella Manyanya akishuhudia pamoja na Nduna Mbano na Magreth Ponera aliye nyuma yake.
Picha ifuatayo Balozi waKwanza wa Makumbusho hayo Inspekta Anna Tembo akisoma taarifa ya Makaribisho wakati waandishi wa habari kutoka kushoto Agustino Chindiye, Moses Konala na muimbaji wa Songea jazzband Sofia wakifuatilia tarifa hiyo kwa makini. Balozi huyo akifurahia zawadi ya faili la Ubunifu toka kwa wajasiliamali wa Ruvuma na baadae akaanza kucheza ngoma ya asili ya WANGONI (BETA) picha ya Mwisho Mweka hazina wa Ruvuma Press Jacquline Moyo kushot akiwa katika pozi na Mjumbe wa Maandalizi ya Chakula cha Kikazi na Balozi Edita Karlo Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania.



No comments:

Post a Comment