Friday, May 28, 2010

Mlezi Mbunge Manyanya anapoteta kuomba umeme!





Kikundi cha Ngoma ya Beta katika viwanja vya makumbusho ya taifa ya Majimaji na kulia Balozi wa Sweden nchini Staffan Herrstom akiangalia ngoma akiwa na Mwenyeji wake Mlezi wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma, Mbunge Stella Manyanya. Picha nyingine balozi akiangalia picha za Mashujaa wa Majimaji ndani ya Jumba la Makumbusho.





Angalia Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club anavyocheza ngoma ya Beta akiwa na kiongozi wa Kundi hilo Mama Nagama,

Pilika za Mapokezi ya Balozi wa Sweden Ruvuma!












Hizi ndio Shangwe na pilikapilika za ujio wa balozi wa Sweden nchini, Mheshimiwa Staffan Herrstom aliyezulu mkoani Ruvuma.
maandalizi hayo yalifanywa kwa ushirikiano kati ya Ruvuma Press Club na Makumbusho ya Taifa ya Majimaji.
Picha ya kwanza Mkurugenzi wa Makumbusho hayo Bw. Philip Maligissu akimkaribisha balozi Herrstom huku Mlezi wa Ruvuma Press Club Mbunge Eng. Stella Manyanya akishuhudia pamoja na Nduna Mbano na Magreth Ponera aliye nyuma yake.
Picha ifuatayo Balozi waKwanza wa Makumbusho hayo Inspekta Anna Tembo akisoma taarifa ya Makaribisho wakati waandishi wa habari kutoka kushoto Agustino Chindiye, Moses Konala na muimbaji wa Songea jazzband Sofia wakifuatilia tarifa hiyo kwa makini. Balozi huyo akifurahia zawadi ya faili la Ubunifu toka kwa wajasiliamali wa Ruvuma na baadae akaanza kucheza ngoma ya asili ya WANGONI (BETA) picha ya Mwisho Mweka hazina wa Ruvuma Press Jacquline Moyo kushot akiwa katika pozi na Mjumbe wa Maandalizi ya Chakula cha Kikazi na Balozi Edita Karlo Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania.



Thursday, May 20, 2010

Mbunge Likokola anapotetea wanawake



Baadhi ya wananchi hudai hawaijui katiba ya nchi wala hawajawahi kuiona. Hivyo hata rangi ya jalada lake hawalijui. hapa Mbunge viti Maalumu Wanawake Mkoa wa Ruvuma Mhe. Devota Mkuwa Likokola, akiinyesha katiba na kuvisoma vifungu katika Mkutano na kueklezea Usawa wa watu na Umuhimu wa kusimamia kikamilifu elimu ya Mtoto wa Kike. Hii ni mifano inayotakiwa kuigwa na viongozi si wa kisiasa tu, bali hata mshirika yasiyo ya kiserikali, Dini, na Wasomi. TGNP wapo mbele kwa kuelimisha. (Picha na Juma Nyumayo)