Monday, January 13, 2014

USIPITWE NA SOMO TOKA KWA SOPHIE LUCAS, SOMA HAPA

  1. Katika kijiji cha Matare wilaya ya
  2. Mugumu Serengeti, bwana
  3. Wambura alikamatwa kwa kesi ya
    kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda
    jela miaka mitatu.
  4. Huku nyuma akiacha mke na
    watoto wanne waliokuwa
    wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa
    sana kichwa chake, alitamani kila
    mtu anayemhisi kuwa ana makosa...
    aingie katika moyo wake na
    kuupata ukweli.
    Alilia na umaskini wake, lambda
    angepata wakili mzuri angeweza
    kumtetea, kumkosa wakili
    kukahalalisha kifungo hicho!!
    Alikwenda gerezani huku akiumia
    sana rohoni. Aliyaanza maisha
    mapya kwa shida sana, akawa
    mnyonge kila mara na mwili
    ukapoteza afya kiujumla.
    Huko gerezani alifanikiwa kupata
    rafiki aliyekuwa na cheo ama
    jukumu la uzikaji wa wafungwa
    hasahasa ambao hawakuwa na
    ndugu ama ambao ndugu zao huwa
    hawajitokezi pale gerezani.
    Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu
    Wambura na kumwaminisha kuwa
    hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha
    anapaswa kuizoea na siku moja
    ukweli utajulikana tu! Bwana
    Wambura maneno ya mzikaji
    hayakumuingia kabisa.. alizidi
    kunyong’onyea.
    “Siwezi kuvumilia kukaa gerezani
    miaka mitatu…..kama unajali kilio
    changu nisaidie nitoroke kwa
    namna yoyote ile ndugu yangu!!”
    Wambura alimsihi mzikaji.
    SIKU MOJA mzikaji akamwambia
    Wambura kuwa msaada
    umepatikana. Lakini yataka moyo!!
    “Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu
    nitoke humu!!” alijibu kwa msisitizo
    huku akimtegea sikio mzikaji.
    “Msaada pekee wa kukutorosha
    humu ndani ni kwa njia ya jeneza…
    yaani mfungwa akifa mimi
    nakuunganisha naye kwenye
    jenerza…..” akashusha pumzi kisha
    akaendelea “Wewe ukisikia kengere
    ya msiba, njoo mara moja kwenye
    chumba cha maiti, utakuta tayari
    sanduku liko katikati ya chumba
    linakuwa halijafungwa, funua
    kifunioko ingia ndani yake ulale
    pembeni ya maiti kwani sanduku
    huwa kubwa la kutosha kila aina ya
    maiti na hata miili miwili inaingia.
    Kisha nitakuja na kulipigilia
    misumari. Baada ya muda
    tutalipakia kwenye gari na kutoka
    kwenda nje ya gereza makaburini
    nikiongozana na baadhi ya
    wafungwa na maaskari magereza.
    Tutakuzika huko lakini baada ya
    dakika 20 hadi 30 nitarudi
    kukufukua. Hautaweza kushindwa
    kupumua kwa dakika hizo, utatoka
    ukiwa huru.”
    JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini
    lilimtisha sana Wambura. Hata
    hivyo akaona afadhali afanye hivyo
    kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
    bila kosa.
    Siku moja akasikia kengere ya
    msiba. Akafanya kama
    alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda
    na kuingia chumba cha maiti. Kweli
    akalikuta sanduku, akiwa na hofu
    kuu akaingia na kulala pembeni ya
    maiti iliyokuwepo. Mara akasikia
    mtu ameingia na kulipigilia
    msumari sanduku. Muda mfupi
    baadaye sanduku likainuliwa na
    kuwekwa kwenye gari.
    Gari ikatoka nje ya gereza hadi
    makaburini. Sanduku likashushwa
    na kuwekwa kaburini na kuanza
    kufukiwa.
    Wambura alijitahidi sana kuvumilia
    japo hofu ilizidi kutanda.
    Alimtegemea sana mzikaji na
    alianza kumuona mkombozi wa
    maisha yake.
    Kama alivyoambiwa, akasubiri
    dakika kumi, ishirini.. zikapita
    kimya!!
    Dakika thelathini kimya. Joto nalo
    likazidi kuongezeka.
    “Nitavumilia hadi afike…”
    alijisemea kisha akajiongezea kauli
    ya ujasiri.
    “Kama nilitakiwa kuishi gerezani
    miaka mitatu kivipi dakika kadhaa
    za hapa kaburini”
    KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
    muda kiasi akatamani kujua
    aliyekufa ni nani… ni kwewli
    aliogopa kuitazama maiti lakini
    aliona kama inatisha zaidi ikiwa
    imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.
    Akaifunua upande wa usoni… Kwa
    kuwa kulikuwa na giza nene
    alikodoa sana macho kuitazama.
    LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
    NA SURA YA MZIKAJI!!!
    MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA
    AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA
    UKOMBOZI!!
    ________________
    FUNZO::
    Usimtegemee sana mwanadamu
    katika maisha yako, kwanza ni
    dhambi!!
    Pili mwanadamu anakumbana na
    vikwazo kama unavyokumbana
    navyo wewe hadi kumwendea yeye.
    Hivyo kumpatia maisha yako ni
    kuzidi kuyaweka hatarini zaidi!!
    Umeonewa umesingiziwa
    unanyanyaswa….. mwachie Mungu
    afanye maamuzi…
    _______________
    Haya mzikaji aliyetegemea
    atamfukua naye ni maiti…… tazama
    mateso atakayoyapata hadi kufa
    kwake…..
    Bila shaka atatamani kurudi
    gerezani kwa miaka mingine kumi
    lakini haitawezekana tena!!!

No comments:

Post a Comment