Friday, November 8, 2013

USTAWI WA KIJAMII NA UCHUMI RUVUMA

Kanisa la RC lililopo Sinai  Manispaa ya Songea, Kanisa hili lipo kando ya barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami toka pacha ya Peramiho kuelekea mjini Mbinga. Eneo hilo sasa limepanda thamani kutokana na usafiri wa uhakika jambo linalovutia wengi kwenda kuwekeza katika kilimo, ujenzi wa nyumba na ufugaji.

Hapa ndiyo "Dar Pori" Wilaya mpya ya Nyasa ni kilomita nane hivi kuingia Msumbiji. Kijiji hiki kimeibuka wakati wa machimbo ya Madini hasa dhahabu. hiyo barabara unayoione imechimbwa kwa majembe ya mkono. hakuna kinachoshindikana kwa binadamu wakidhamiria. Vijana wa bodaboda maarufu kama yeboyebo mkoani Ruvuma wakisubiri abiria "waliobongoa" waliopata fedha au madini  kuwapeleka Mbinga, Nauli yake ni Shs 40,000/- kwa abiria mmoja. Kazi kwelikweli. 

Mkazi wa Dar es Slaam, Bw. Jacob Silvesta Nyumayo, akionyesha mkungu wa ndizi huko kijiji cha Mgazini Kata ya Kilagano Songea Vijijini ambao umezaa vya kutosha licha ya kutotunzwa vizuri. Bw. Jacob anasema udongo wa Songea unafaa sana kwa kuzalisha ndizi za aina zote na huenda ndizi zingeliweza pia kuchangia pato la wananchi wa mkoa wa Ruvuma wakithubutu hasa wakati huu ambao sasa barabara zimefunguka na kuacha kutegemea zao moja tu la chakula kama mahindi na kutupilia mbali mihogo, mtama na mazao mengine. 

No comments:

Post a Comment